NA KALUME KAZUNGU WAGENI na watalii waliohudhuria tamasha za utamaduni wa Lamu mnamo Jumapili waliendelea kukaa katika hoteli na gesti kisiwani Lamu baada ya shughuli za usafiri kukatizwa na mafuriko katika eneo la Gamba kwenye barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen. Hafla ya utamaduni wa Lamu iling’oa nanga mnamo Alhamisi wiki iliyopita na kukamilika rasmi Jumamosi usiku. […]