NA SAMMY WAWERU MSITU Kirisia, ulioko Maralal, Samburu uliwahi kuvamiwa na maskwota kutoka eneo hilo. Jamii inayoishi humo ikiwa ni wafugaji wa kuhamahama, ilikuwa imeunda manyatta – makazi maalum, miti ikaangushwa, baadhi wakiingilia shughuli ya uchomaji makaa na kilimo. Maliasili iliharibiwa, msitu uliokuwa chanzo cha chemichemi za maji na mvuto wa mvua ukawa hauna thamani […]