NA LUCY MKANYIKA GAVANA wa Taita Taveta, Andrew Mwadime, amesema kuwa ataanzisha chama chake cha kisiasa ambapo yeye atakuwa kinara. Akiongea wakati wa mkutano wa wajumbe wa ODM uliofanyika katika hoteli ya Panlis, Mwatate, Bw Mwadime alisema ataanzisha chama chake baada ya msukosuko aliokabiliana nao katika uchaguzi uliopita, 2022. Mkutano huo ulihudhuriwa na kinara wa […]