WAHUDUMU wa huduma ya chakula jijini Arusha wametakiwa kuongeza matawi katika jiji hilo ili kuongeza kasi ya uwepo wa chakula vitakavyovutia watalii jijini humo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ametoa rai hiyo leo Februari 13, 2024 wakati wa uzinduzi wa mgahawa wa KFC na kuwataka kuongeza matawi zaidi mkoani hapo ili kuwezesha wananchi wanaotumia huduma za vyakula kuvipata kwa ukaribu.

RC Mongela amesema huduma bora ya chakula ni muhimu kutolewa Arusha ili kuwavuta zaidi watalii na wananchi kwa ujumla kupata vyakula vya uhakika na kuomba KFC kufunga matawi mengine zaidi jijini humo.

“Tunashukuru kufika Arusha lakini naomba muongeze zaidi migahawa yenu maana Arusha ni jiji la kitalii lakini pia nashukuru ajira kwa vijana vinakua kutokana na bidhaa mzazouza ikiwemo serikali kupata mapato.” Amesema

Akimzungumzia uamuzi wa kufunguka KFC jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works,Vikram Desai amesema hiyo ni hatua muhimu kwa Tanzania kuwafikishai wananchi huduma bora ya chakula lakini pia inachagia ajira kwa watanzania

Mkurugenzi wa kampuni ya Oryx Energies Tanzania,Kalpesh Mehta ameongeza kuwa kampuni hivyo imejipanga kuhakikisha Tanzania inashirikiana na kampuni ya Dough Works Tanzania katika kuhakikisha huduma ya KFC inatolewa kwa ufanisi ambapo Meneja masoko wa KFC ,Lyse Mosha ametoa ombi kwa wakazi wa Arusha kutumia vyakula vinavyouzwa kwenye migahawa huyo iliyopo nchini.

The post Wahudumu wa chakula Arusha waongeze matawi-Mongella first appeared on HabariLeo.