Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

Jukwaa la Mavazi la Laady in Red, linalofanyika kila Mwaka hususan msimu wa wapendanao linatarajiwa kufanyika Februari 12, katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo linaandaliwa na kampuni ya Hugo Domingo kwa mwaka wa pili huu, linalenga kuinua na kuibua vipaji vya wabunifu wachanga na wanamitindo nchini.

Akizungumza na waandishi waa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 26, 2022 Mratibu wa Tamasha hilo, Merry Fernandez, amesema mwaka huu litakuwa na tofauti kubwa ikilinganishwa na mwaka jana.

“Tasnia ya mitindo inazidi kukuwa hivyo wabunifu kila kukicha wanaibua kitu kipya kupitia Lady in red mwaka huu kutakuwa na stayle mpya za mavazi kwa kuwa wote waliojisajili ni wabunifu makini,” amesema Merry.

Kwa upande wa Muasisi wa tamasha hilo, Asia Idarus Hamsini ameiomba Serekali kutupia jicho la tatu katika tasnia ya mitindo kupitia jukwaa hilo ili kusaidia wabunifu.

“Naiomba serekali kuangalia wabunifu wapya ambao tuna waibua kupitia Lady in Red kwa kuwapatia mitaji ili kukuza biashara zao ukizingatia tasnia ya mitindo imekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa,” amesema Asia.