Match reports, transfers and results from East African football and leagues worldwide, plus athletics, basketball and the biggest stories in global sport.
Salamata Kouanda amefunga magoli manne katika ushindi wa 7-1 iliyoupata Yanga Princess dhidi ya Kilimanjaro Wonders, mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Magoli…
Atletico Madrid have hit back at Jose Mourinho after the Real Madrid manager accused referees of making key errors during Sunday’s Madrid derby defeat.
The United Kingdom, UK has changed the eligibility rules for overseas-trained teachers seeking to obtain Qualified Teacher Status (QTS) in England, removing Nigeria, Ghana and India from the countries whose teachers can use the direct application service.
UONGOZI wa Kagera Sugar, umefikia makubaliano ya pande mbili kuachana na Kocha Mkuu, Juma Kaseja kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa matokeo ya timu hiyo katika michezo sita ya Ligi Kuu Bara msimu huu.
HOPE City Deaf imeanza kupata matumaini katika Ligi ya Viziwi Zanzibar baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Zandeaf, katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bakari Selemani Msimu japokuwa haanzi moja kwa moja kikosi cha kwanza, lakini amesema hiyo siyo sababu ya kuacha kujifunza vitu muhimu vya kumjenga kuwa mchezaji mkubwa na tegemeo kwa baadaye.
MASHUJAA FC imegeuza breki ya FIFA kuwa fursa ya kurekebisha upungufu uliojitokeza kwenye mechi za mwanzo za msimu, huku kocha Amani Josiah akipanga kuimarisha safu ya ulinzi na kuongeza makali kwenye ushambuliaji.
Je, tayari umechagua mechi zako kwa ajili ya mkeka wa aina ya 'accumulator'? MELBET ina kitu maalum kwa ajili ya mkeka wako! Kipengele cha 'Accumulator Booster' huongeza bonasi kwa kuzidisha jumla ya 'odds' zako.
Cole Palmer has withdrawn from England's squad because of a muscle injury, with Nottingham Forest midfielder Morgan Gibbs-White set to replace the Chelsea star, according to Sky Sports.
YULE mshindi atakayeuwakilisha Ukanda ya Afrika Mashariki na Kati kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana AFCON U-20 anapatikana leo kwenye mechi za nusu fainali.
UTANGULIZI “Nilihitaji malezo kwa ufupi, hebu niambie nini kilitokea?” Amour akaelezwa kilichokuwa kimetokea. “Hao watu walikuwa wamevaa nguo za rangi gani?” Akauliza. “Mmoja alivaa nguo za rangi nyeusi, wengine wawili walivaa nguo za rangi nyeupe.” Hapo hapo Amour akaamini kwamba wauaji walikuwa ni wale wale waliokuwa wakiwaua watoto wa Almasi. “Huyo aliyevaa nguo nyeusi yukoje?” Amour aliendelea kuuliza. “Kusema ukweli hatukuwaona vizuri.” SASA ENDELEA... “Namfananisha na mtu mmoja ambaye anaonekana kama vile shingo yake imechinjwa.” “Kusema kweli huyo mtu ndivyo alivyokuwa akionekana. Kichwa chake kilikuwa kinaning’inia.” Hao ndio wauaji wale wale wa watoto wa Almasi! Amour akajiambia kimoyomoyo. Alijiambia kudhani kwake kuwa alikuwa amewakamata majambazi hao kulikuwa sivyo kabisa. Aliowakamata walikuwa majambazi wengine. Amour akajiuliza atakwenda kumueleza nini Mkurugenzi wa Upelelezi kuhusiana na kuuawa kwa kijana huyo? Alijiuliza hivyo baada ya kufahamu kuwa alishamueleza kuwa majambazi waliokuwa wameiandama familia ya Almasi alikuwa amewakamata na wengine kuwaua. “Lakini yule mganga alikiri kuwapa dawa za uchawi majambazi wale!” Amour alikuwa akiendelea kusema na moyo wake. Wakati huo akizungumza na polisi wa benki kwenye simu alikuwa amenyamaza kidogo akitafakari. “Natumaini umenielewa afande?” Sauti ya upande wa pili wa simu ikamuuliza Amour. “Nimekuelewa isipokuwa muhakikishe kuwa kesho mnafika hapa kuandikisha maelezo yenu.” Amour alikata simu na kumtazama mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze ambaye naye alikuwa akimtazama. “Kama hawa askari watakuja hapa Chalinze kesho hakikisha unaandikisha maelezo yao na kisha uniletee ofisini kwangu,” akamwambia. “Nitafanya hivyo.” Ndipo Amour na makachero wenzake walipoanza ,msafara wa kurudi Dar wakiwa na mwili wa John. Gari la John halikuachwa Chalinze. Kulikuwa na polisi mmoja aliyeliendesha kulipeleka Dar. Walipofika Dar es Salaam mwili wa John ulipelekwa hospitali ya Muhimbili. Gari la marehemu liliachwa katika eneo la kuegesha la makao ya polisi. Baada ya kuupeleka mwili wa John hospitalini Amour alirudi ofisini kwake na kumpigia simu mzee Almasi. “Inspekata habari yako?” Sauti ya Almasi ikasikika kwa uchangamfu mara tu simu ilipopokelewa. “Nzuri Bwana Almasi. Uko wapi?” “Hapa niko ofisini Mikocheni. Kuna tatizo lolote?” “Ninakuhitaji ofisini kwangu.” “Nije ofisini kwako?” “Ndiyo. Kuna tatizo limetokea.” “Tatizo gani tena. Mwanangu ameenda Arusha kwenye mkutano. Kulikuwa na kazi ameziacha, ninazimalizia.” Amour aliposikia kauli hiyo aligutuka na kumuuliza. “Mwanao gani aliyekwenda Arusha?” “John. Ameondoka asubuhi kwenda Arusha, kwa hiyo imebidi nimshikie ofisi yake hadi atakaporudi.” “Sawa, sasa acha kazi uliyonayo uje mara moja, kuna kitu muhimu.” “Sawa. Ninakuja.” Amour akakata simu huku akijua kuwa John aliyemtaja Almasi ndiye yule aliyeuawa. Alijiuliza atawezaje kumueleza baba yake kuwa mwanawe ameuawa njiani wakati akielekea huko Arusha? Aliogopa kwamba angemshitua kumjulisha kuwa mwanawe huyo ameuawa. Lakini pia kauli yake ingemsuta mwenyewe kwa sababu alishamhakikishia Almasi kuwa wauaji wa watoto wake alishawakamata. Amour alitikisa kichwa peke yake kusikitika. Almasi aliondoka ofisini akiwa hajui kilichotokea. Alijipakia kwenye gari lake akaondoka kuelekea makao ya polisi. Wakati analiegesha gari kwenye eneo la kuegesha la makao ya polisi alishituka allipoliona gari la ,mwanawe John likiwa limeegeshwa mahali hapo. Aliposhuka kwenye gari alikwenda kuliangalia vizuri akahakikisha lilikuwa ni gari na mwanawe John ambalo aliondoka nalo asubuhi kuelekea Arusha. “Limefikaje hapa?” Akajiuliza. “John mwenyewe yuko wapi?” Akaendelea kujiuliza bila kupata jibu. Alipogeuka nyuma alimuona polisi mmoja akiwa na hamsini zake, akamuita. Polisi huyo alipofika alimuuliza. “Hili gari la mwanangu, limefikaje hapa?” “Nenda ukawaulize wanaohusika humo ndani.” Ndilo lililokuwa jibu la polisi huyo. Almasi akawa ameanza kuchanganyikiwa. Baada ya kusita sita kwa sekunde kadhaa akilitazama gari hilo, aliondoka kuelekea ofisini kwa Inspekta Amour. “Karibu kiti.” Amour alimwambia mara tu alipomuona akiingia ofisini kwake. Almasi hakukaa kwenye kiti. “Nimeona gari la mwanangu John hapo nje, kumetokea nini? Na John mwenyewe yuko wapi?” “Kaa kwenye kiti. Nimekuita kukueleza matatizo ya mwanao John. Naomba unisikize kwa makini.” Almasi alikaa lakini alikuwa ameshakosa amani. Amour alianza kumueleza jinsi alivyopigiwa simu kutoka kwa mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze na kuarifiwa kuhusu mtu aliyeuawa huko Wami. “Tulifika Chalinze tukaouona mwili wa mtu huyo ambao ulikuwa umeshafikishwa hospitalini. Tuliona pia na gari lake. Nikagundua kuwa mwili huo ulikuwa ni wa John pamoja na hilo gari uliloliona hapo nje.” Uso wa Almasi ulianza kubadilika rangi. Mwanzo ulikuwa mweusi sasa ukawa mwekundu. “Tulivyoelezwa na polisi ni kwamba gari la John lilipata pancha lilipofika Wami. John akalisimamisha pemebeni mwa barabara na kudadili tairi lakini hapo hapo walitokea watu ambao walimchinja na kutoweka.” Amour alinyamaza akamtazama Almasi kuona jinsi alivyokuwa akiyapokea maelezo yake. “Unataka uniambbie kuwa mwanangu John naye amechinjwa?” Almasi akauliza kwa sauti ambayo haikuwa tulivu hata chembe. “Ukweli ndio huo na inabidi tukueleze kilichotokea. Kulikuwa na polisi wawili waliokuwa katika gari jingine ambao waliona hilo tukio. Lakini waliposimamisha gari ili kutoa msaada, watu hao walitoweka ghafla.” “Hao wauaji ni kina nani?” “Hatujawafahamu na tunaendelea na uchunguzi.” “Inspekata uliniambia kuwa umeyakomesha mauaji ya watoto wangu na kwamba majambazi waliohusika umeshawakamata!” “Tunafanya uchunguzi kujua kama wauaji ni wale wale au ni wengine.” “Haiwezekani wawe ni wale wale wakati ulishawakamata.” “Ndio tunafanya uchunguzi ili tuweze kujua. Tukio lenyewe limetokea mbali. Tumefanya kuarifiwa na polisi wenzetu. Kesho tunatarajia polisi walioshuhudia tukio hilo watafika hapa ili tuweze kuwahoji.” “Unajua sielewi chochote unachonieleza. Nataka kwanza niuone mwili wa mwanangu, John uko wapi?” “Uko hospitali ya Muhimbili.” “Naomba kwenda kuuona.” Dakika chache baadaye, Amour na Almasi wakiwa katika magari tofauti walikuwa njiani kuelekea hospitali ya Muhimbili. Amour alikuwa akiendesha kwa umakini lakini haikuwa hivyo kwa Almasi ambaye taharuki lilimfanya atetemeke mwili mzima. Presha ilikuwa juu na alikuwa akifoka peke yake akimlaumu Inspekta Amour. Walipofika Muhimbili walikwenda mochwari ambapo walitolewa mwili wa John. Almasi aliuona akaangua kilio. Alitoa kitambaa akaufuta uso wake kisha kwa macho yaliyokuwa mekundu alimtazama Amour. “Unanieleza nini kuhusu kuuawa kwa mwanangu?” Akamuuliza. “Tutatoa taarifa yetu baada ya uchunguzi wetu kukamilika.” “Ni kwanini watoto wangu wanauawa ovyo?. Huo uchunguzi wenu utakamilika lini?” “Jaribu kutuliza hasira mzee wangu. Sisi pia tunasikitika kuona watu wetu wanauawa kila siku na tunahangaika usiku na mchana kuhakikisha usalama wa watu wetu….” “Lakini wewe hushangai kuona watoto wangu wanaandamwa namna hii? Mtu alikuwa anaenda safari anafuatwa na kuuawa bila sababu. Kama walitaka pesa au gari si wangechukua tu na kumuacha mwanangu! Ukatili gani huu?” Amour alitikisa kichwa. “Umeouona mwili wa mwanao, naomba turudi ofisini.” alimwambia Almasi aliyeonekana kuchanganyikiwa. Waliporudi tena ofisini, Amour alimuuliza Almasi kama marehemu alikuwa na kiasi chochote cha pesa ndani ya gari. “Alikuwa amechukua pesa za matumizi yake tu akiwa huko Arusha. Hakuwa amechukua pesa nyingi. Sijui walimuua kwa sababu gani?” “Sisi tulikuta shilinggi milioni moja kwenye mifuko yake pamoja na vitu vyake vingine ambavyo tutakukabidhi.” “Shilingi milioni mmoja zitanisaidia nini mimi wakati roho ya mwanangu imeshatoka, amelala kama walivyolala kaka zake.” Almasi alisema kisha alitoa kitambaa na kuufuta uso wake uliokuwa umetota. Amour aliona alikuwa amekabiliwa na wakati mgumu kuelewana na mtu huyo wakati ule. Alijiambia alipaswa amruhusu aende zake kisha amuite wakati mwingine atakapokuwa ametulizana na kuzungumza naye. “Sasa mzee Almasi unaweza kurudi nyumbani ukatoe taarifa kwa ndugu na jamaa. Nadhani baada ya maziko nitakuita tena.” Amour alimwambia Almasi. Almasi aliinuka kwenye kiti huku akilia kama mtoto mdogo. Kitambaa kilikuwa kwenye uso wake. Amour alimbembeleza na kutoka naye ofisini. Alimuagiza polisi mmoja amsindikize hadi nyumbani kwake. Aliporudi tena ofisini kwake simu yake ikaita. Alipotazama namba inayompigia akaona namba za Mkurugenzi wa Upelelezi. Akajua kuwa bosi wake alikuwa anampigia baada ya kupata taarifa ya mauaji ya mtoto mwingine wa Almasi. Siku chache tu zilizopita, Amour alimwambia bosi wake huyo kuwa aliwakamata watu waliokuwa wakiwaua watoto wa Almasi na bosi huyo aliamini kuwa tatizo hilo lilikuwa limekwisha.
DAR ES SALAAM. KOCHA Msaidizi wa JKT Tanzania, George Mketo, amesema timu hiyo inatumia mapumziko ya kalenda ya FIFA kwa kufanya maandalizi ya nguvu kwa michezo iliyo mbele ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza na DailyNews Digital kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuhyo Dar es Salaam leo Septemba 21, 2026, amesema kuwa benchi la ufundi limeweka…
Ghana star Antoine Semenyo scored twice for Manchester City, whose 5-3 victory over Sunderland took them to the top of the Premier League table at the weekend.
Tanzania imepangwa Kundi B pamoja na Misri, Angola na Msumbiji katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika la Futsal 2026, ambazo zimepangwa kufanyika Morocco kuanzia Oktoba 12 hadi 23 mwaka huu.
Tanzania imepangwa Kundi B pamoja na Misri, Angola na Msumbiji katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika la Futsal 2026, ambazo zimepangwa kufanyika Morocco kuanzia Oktoba 12 hadi 23 mwaka huu.
Kambi ya Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania ' Taifa Stars', imepata nguvu zaidi, baada ya Kibu Denis na Syprian Kachwele kuwasili na kuungana na wenzao, lakini wakati nyota hao wakianza kuipa hamasa timu, mpango wa kukutana na Ghana umevunjika.
SPAIN: THE Minister for Information, Culture, Arts and Sports, Paul Makonda, has invited FC Barcelona stars to visit Tanzania as part of the ongoing strategic campaign to inspire youth and promote the 2027 Africa Cup of Nations (AFCON) finals. During a high-profile tour of the Catalan club’s historic headquarters, Makonda met with several first-team players,…
ZANZIBAR: ZANZIBAR President Dr Hussein Mwinyi has said the government will continue working closely with religious institutions to safeguard peace and national unity, describing faith leaders as indispensable partners in advancing Tanzania’s development. Speaking yesterday during the consecration and installation of the 11th Bishop of the Anglican Church’s Diocese of Zanzibar, Bishop Lameck Paul Ndomba,…
Ferran Torres continued the impressive start to his PsG career by scoring the opener as the French and European champions won 2-1 at bitter rivals Marseille in Ligue 1 on Sunday.
Michael Carrick insisted that there were positive signs from Manchester United's 1-1 draw at Fulham after Matheus Cunha saved his side from a third successive defeat on Sunday.
Manchester United rescued a 1-1 draw against Fulham thanks to Matheus Cunha's late equaliser on Sunday, but the pressure is mounting on boss Michael Carrick after their latest lacklustre display.
The President said Kaduna’s experience demonstrated what was possible when subnational governments deployed alternative energy to provide affordable transportation.
Manchester City moved to the top of the Premier League in explosive style as Enzo Fernandez's first goal for the club lit the fuse on a pulsating 5-3 win against Sunderland on Sunday.
KOCHA Mkuu wa Zimamoto, Abdallah Mohammed ‘Bares’ amesema kutokana na malengo yake ya kuhitaji ushindi kila mechi anayocheza, amekuwa akiingia kwa mitindo tofauti ili mpinzani asimsome kirahisi.
KATI ya mechi nane ambazo KVZ imecheza msimu huu za mashindano tofauti, imeonekana kutokuwa kwenye kiwango kizuri, huku shida ya matokeo hayo ikibainika kwenye maeneo mawili ambayo ni ulinzi na ushambuliaji.
UTANGULIZI Alikaza nati ya kwanza kisha akaanza nati ya pili. Wakati anaitia spana kwenye nati ya tatu akahisi kitu chenye makali kikimtekenya shingoni mwake. Akashituka na kugeuza uso. Akamuona mtu aliyekuwa amevaa mavazi meusi nyuma yake akiwa amemshikia panga lililokuwa limesogezwa kabisa kwenye shingo yake. Cha kutisha zaidi ni kuwa shingo ya mtu huyo ilikuwa imechinjwa na kufanya kichwa chake kiwe kinaning’inia kama kilichotaka kuanguka! Upande wa kulia na wa kushoto wa mtu huyo kulikuwa na watu wengine wawili waliovaa mavazi meupe. SASA ENDELEA... Hapo hapo ile picha ya mauaji ya kaka zake Martin na James ikamjia akilini. Wauaji wao walielezwa kuwa walikuwa watatu kama wale waliokuwa pale. Mmoja alikuwa amevaa mavazi meusi na wengine wawili walivaa mavazi meupe. Kwa jinsi allivyoshituka na kugwaya, John alishindwa hata kuwauliza wale watu walikuwa kina nani na walitaka nini lakini akilini mwake alikumbuka kwamba watu hao walikuwa majambazi na walishakamatwa na wengine kuuawa. Umbali wa kilometa moja hivi kulikuwa na gari la benki lililokuwa linakuja kutoka Dar likiwa na pesa za benki. Lilikuwa na maafisa wawili wa benki ya Handeni pamoja na polisi wawili waliokuwa na bunduki. Kwa vile barabara ilikuwa imenyooka, waliliona gari la John lililokuwa limepata pancha likiwa pembeni mwa barabara. Walimuona pia John aliyekuwa akibadili tairi. Lakini ghafla waliwaona watu watatu, wawili wakiwa na mavazi meupe na mmoja akiwa na mavazi meusi ambao walimvamia John. Aliyevaa mavazi meusi alikuwa ameshika upanga. “Wewe ni mtoto wa Almasi?” Mtu aliyekuwa amevaa mavazi meusi ambaye kichwa chake kilikuwa kinaning’inia alimuuliza John. “Ndiyo. Mimi ni mtoto wa Almasi.” John alijibu haraka na kwa kubabaika kama vile alihisi akikubali kuwa yeye ni mtoto wa Almasi angesalimika. Gari la benki llilikuwa limeshafika karibu. “Baba yako alikuweka kama dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamna yako…” Mtu huyo aliendelea kumwambia John. “Dhamana gani?” John akauliza akiwa amemkazia macho mtu huyo aliyekuwa akitisha. “Huwezi kupata jibu kwa sababu muda wako wa kuishi umeshakwisha!” “Yesu wangu…!” Hapo hapo upanga ukapita kwenye shingo ya John. Koo lilikatwa, damu ikamwagika kama maji ya bomba. Martin akarudi chini taratibu akiwa maiti. Gari la benki liliwapita kabla ya kusimama. Wale polisi waliokuwa na bunduki walishuka haraka. Walipotupa macho hawakuwaona tena wale watu watatu bali walimuona John akiwa amelala chini huku damu ikimtoka shingoni. Polisi hao walitupa macho kila upande kuwaangalia watu hao lakini hawakuwaona tena. Polisi mmoja akasogea pale ilipokuwa maiti ya John na kugundua kuwa John alikuwa amechinjwa na tayari alikuwa ameshakufa akarudi na kumfahamisha polisi mwenzake pamoja na wale maafisa wa benki. “Kwa hiyo wale watakuwa majambazi?” Mmoja wa maafisa hao wa benki akamuuliza. “Watakuwa ni majambazi. Wamemchinja yule kijana kisha wamekimbia.” “Sasa walitaka nini? Walitaka kuiba lile gari?” Afisa mwingine wa benki akauliza. “Inawezekana walimuua ili waibe gari au pesa lakini walipotuona sisi wakakimbia.” “Wamemchinja kabisa?” “Wamemchinja na ameshakufa.” “Sasa tufanyeje?” “Tuwaarifu polisi wenzetu wa Chalinze waje hapa mara moja halafu sisi tuendelee na safari yetu. Au mnaonaje?” “Ni sawa. Tutasubiri kidogo. Aliyeuawa ni binaadamu mwenzetu.” Afisa mmoja wa benki alisema. Polisi huyo akatoa simu na kuwapigia polisi wa Chalinze. “Kuna tukio la mauaji limetokea hapa mbele ya daraja la Wami” Polisi huyo alimwambia mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze baada ya kujitambulisha. Akaongeza “Tulikuwa tunatokea Dar tukisindikiza pesa za benki kuelekea Handeni, tukalishuhudia tukio hilo likitokea mbele yetu.” “Sasa nani ameuawa na ilikuwaje?” Mkuu wa kituo hicho akauliza kwa sauti ya taharuki. Polisi huyo akamueleza tukio hilo lilivyotokea. “Umesema mtu huyo amechinjwa na wachinjaji hao wamekimbia?” “Amechinjwa na bado tuko naye hapa. Hao wachinjaji walikimbia baada ya kkutuona sisi.” “Kwa hiyo mlishuhudia hilo tukio?” “Ndiyo tulilishuhudia.” “Na bado mko katika eneo hilo?” “Bado tupo hapa. Tunawaomba mfike haraka ili tuweze kuendelea na safari.” Pakatokea ukimya kidogo upande wa mkuuu wa kituo cha polisi cha Chalinze. “Nadhani umenielewa afande?” Polisi huyo aliyepiga simu akauliza. “Nimekuelewa.” “Sasa naomba mfike haraka. Unajua tuna fedha za benki na tupo mahali pa hatari!” “Sawa. Tunakuja.” Dakika kadhaa baadaye gari la polisi kutoka Chalinze likawasili mahali hapo. Lilikuwa na polisi sita, watatu wakiwa na bunduki. Waliposhuka kwenye gari walikutana na polisi wenzao ambao walikwenda kuwaonesha maiti ya John. “Mtu mwenyewe ni huyu hapa.” Polisi mmoja wa benki akawambia polisi hao. “Loh…amechinjwa kweli!” Mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze ambaye alikuwemo kwenye msafara huo wa polisi alimaka baada ya kuiona maiti hiyo. “Tunadhani kwamba gari lake lilipata panchari na alikuwa amebadili tairi ya gari kabla ya kuvamiwa na watu hao.” Polisi wa benki aliendelea kueleza. “Hao watu walikimbillia upande gani?” Mkuu huyo wa kituo akauliza. “Hatukuwaona upande waliokimbilia.” “Si mliniambia kuwa mlilishuhudia tukio la kuuawa kwake?” “Tulilishuhudia tukiwa kwenye gari lakini tuliposimamisha gari hao watu hatukuwaona.” Polisi hao wa kituo cha Chalinze wakaanza uchunguzi. Walilikagua lile gari huku wengine wakiukagua mwili wa John pamoja na kumpekua. Walikuta hati kadhaa ndani ya gari na pia walipata kitambulisho cha John pamoja na fehda zilizokuwa mfukoni mwake na kwenye mkoba wake uliokuwa ndani ya gari. “Kwa vile nyinyi ndio mashahidi pekee wa tukio hili ningependa kupata majina yenu.” Mkuu huyo wa kituo aliwambia. Baada ya kuandikisha majina ya polisi walioshuhudia tukio hilo pamoja na namba zao za simu, waliandikisha pia majina ya wale maafisa wa benki pamoja na namba zao. “Sasa pelekeni pesa ila ninawaomba kesho mfike kituoni kwetu Chalinze muandikishe maelezo yenu.” Baada ya kukubaliana hivyo polisi waliokuwa wakisindikiza pesa za benki waliondoka. Polisi wa kituo cha Challinze waliubeba mwili wa John na kuupakia kwenye gari lao kisha wakabadili ile tairi iliyopata panchari. Baada ya kuweka tairi nyingine wakaliwasha gari la John. Gari hilo lilipowaka wakaondoka nalo. Kitambulisho kilichopatikana mfukoni mwa John kilionesha kwamba alikuwa mkazi wa dar es Salaam na meneja wa kiwanda cha maji safi cha Almasi. Walipofika Chalinze, polisi hao waliupeleka mwili wa John hospitali kisha wakawapigia simu polisi wa Dar es Salaam na kuwaarifu kuhusu tukio hilo. Baada ya kupata habari kuwa kitambulisho cha mtu aliyeuawa huko Wami kina jina la John Almasi, mkazi wa Dar es Salaam na meneja wa kiwanda cha maji safi cha Almasi, haraka Inspekta Amour pamoja na polisi wengine wanne waliondokana gari kwenda Chalinze. Walipofika walipelekwa hospitali ambako mwili wa John ulikuwa umehifadhiwa. Alipouona tu mwili huo, Amour akautambua kuwa ulikuwa mwili wa mmoja wa watoto wa Almasi kwani alikuwa akiwafahamu. Kitendo cha kumshuhudia mmoja wa watoto wa Almasi akiwa amechinjwa kilimshitua. Ingawa mara kwa mara alikuwa amezoea kuwashuhudia watu waliouawa, kwa mtoto wa Almasi mshituko wake ulikuwa mkubwa. Si kwa sababu tu alikuwa amechinjwa bali kabla ya tukio hilo alikuwa akiamini kwamba alikuwa ameyatokomeza mauaji ya kikatili yaliyoiandama familia ya Almasi baada ya kuwakamata majambazi aliohisi kuwa ndio waliokuwa wakiendesha mauaji hayo.. “Ninamfahamu ni mtoto wa Bwana mmoja mwenye kiwanda cha maji safi anayefahamika kwa jina la Almasi huko Dar.” Amour alimwambia mkuu wa kituo cha polisi cha Chalinze kabla ya kumuuliza. “Kuna maelezo uliyopata kuhusu kuuawa kwake?” “Sisi tuliarifiwa na polisi wenzetu waliokuwa wakisindikiza pesa za benki wilaya ya Handeni. Tulipokwenda kuuchukua mwili huo pamoja na gari la marehemu, tuliwambia wafike kesho kuandikisha maelezo yao.” “Ningehitaji nipate maelezo hata hii leo. Umechukua namba zao za simu?” “Namba zao ninazo.” “Nipatie.” “Zipo ofisini.” “Twende ukanipatie. Ninazihitaji.” Walikwenda kituoni hapo ambapo Amour alikaa ofisini mwa mkuu wa kituo hicho na kupatiwa namba za simu za polisi walioshuhudia tukio hilo. Mara tu alipopewa namba hizo, Amour alimpigia polisi mmojawapo. “Unazungumza na Inspekta Amour wa makao ya polisi jijini Dar lakini kwa sasa niko Chalinze. Tumepata taarifa ya mauaji yaliyotokea hapo Wami na tumeambiwa kuwa wewe na polisi mwenzako mlishuhudia tukio hilo wakati mkiwa kwenye gari mkielekea Handeni.” “Ndiyo afande tulishuhudia.” “Nilihitaji malezo kwa ufupi, hebu niambie nini kilitokea?” Amour akaelezwa kilichokuwa kimetokea. “Hao watu walikuwa wamevaa nguo za rangi gani?” Akauliza. “Mmoja alivaa nguo za rangi nyeusi, wengine wawili walivaa nguo za rangi nyeupe.” Hapo hapo Amour akaamini kwamba wauaji walikuwa ni wale wale waliokuwa wakiwaua watoto wa Almasi. “Huyo aliyevaa nguo nyeusi yukoje?” Amour aliendelea kuuliza. “Kusema ukweli hatukuwaona vizuri.”
Coventry City striker Taiwo Awoniyi has been called up to replace injured Victor Osimhen in Nigeria’s squad for the 2027 Africa Cup of Nations qualifiers against Madagascar and Guinea Bissau.
Canada has introduced category-based selection under its Express Entry immigration system to help the country attract candidates with skills and experience in areas linked to specific economic needs.
Uongozi wa Klabu ya Gymkhana ya Dar es Salaam, Dar es Salaam Gymkhana Club (DGC) umemzuia mwekezaji aliyejenga viwanja vya mchezo wa Racket, kampuni ya East Africa Racket Sports Club Limited (EARSC), kuendelea na shughuli hizo.
MZIMU wa majeraha umeendelea kuitesa Kagera Sugar baada ya wachezaji sita wa kikosi hicho kukumbwa na kadhia hiyo, huku mshambuliaji, Kassim Fekha huenda akakosekana msimu huu mzima wa 2026-2027. Nyota huyo amefanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuumia katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida Black Stars iliyochezwa Agosti 19, 2026, jambo litakalomwweka nje kwa takribani miezi saba hadi tisa. Akizungumza na Mwanaspoti, Daktari wa Kagera Sugar, Abel Shindika amesema mchezaji huyo aliumia vibaya walipocheza dhidi ya Singida Black Stars, japo tayari amefanyiwa upasuaji na atakuwa nje kwa muda wa miezi saba hadi tisa. "Ni kipindi kigumu sana kwetu sisi benchi la ufundi na mchezaji mwenyewe kwa sababu ni mtu muhimu sana kikosini, awali ilionekana ni jeraha dogo tu lakini baada ya vipimo tukagundua ni kubwa na kumfanyia upasuaji huo," amesema Shindika. Aidha, Shindika amesema mwingine ni kiungo wa kati wa timu hiyo, Freddy Tangalo ambaye kwa sasa atakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili, baada ya kuvunjika mfupa wa paja katika mechi dhidi ya maafande wa Mashujaa FC, Agosti 27, 2026. "Wachezaji wengine ni Said Kipao, Abdul Mohamed na Ally Salum wanaosumbuliwa na kifundo cha mguu na baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA watarejea, huku, Deus Malilo akiuguza majeraha ya goti," amesema. Kwa upande wa meneja wa kikosi hicho, Bernard Samson Sikira, amesema wakati wa kipindi hiki cha mapumziko wanaendelea na kupambana kwa ajili ya kupata vibali vya wachezaji watatu wa kimataifa, ambao wameshindwa kuonekana hadi sasa uwanjani. Wachezaji hao ni beki wa kati, Boniface Onyango kutokea Kakamega Homeboyz ya kwao Kenya, kiungo mshambuliaji, Emmanuel Mvuyekule aliyetokea Vision FC ya kwao Burundi na mshambuliaji Mkenya Collins Maina aliyetoka Fortune Sacco FC. Kagera inayofundishwa na Kocha Mkuu, Juma Kaseja imeanza vibaya msimu wa 2026-2027, kwani tangu ipande daraja, imecheza mechi sita za Ligi Kuu Bara na kati ya hizo imetoka sare mbili na kuchapwa nne, ikiwa nafasi ya 15 na pointi mbili.
MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, Maulid Shaban amesema kucheza timu moja na Mzambia Obrey Chirwa ni jambo nzuri ndani ya kikosi hicho, ingawa ni changamoto pia kwake, kutokana na ushindani wa nafasi.
TIMU ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes imeendelea kuonyesha ubora mkubwa kwenye mashindano ya CECAFA U-20 yanayoendelea hapa nchini.
KOCHA wa timu ya Taifa ya U-20 ya Ethiopia, Benjamin Ziemer amesema vijana wake walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga dhidi ya Tanzania, lakini walishindwa kuzitumia vizuri hali iliyowagharimu katika mchezo huo wa kufuzu AFCON U-20.
WAKATI wewe unapita zako YouTube kushangaa video za vichekesho na nyimbo za wasanii mbalimbali, Winga Mtanzania, Bernard Kamungo aliutumia mtandao huo kujifunza lugha.
KIUNGO mshambuliaji wa Tanzania, Nasma Manduta amesaini mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya Antalya Spor ya Uturuki akitokea Ceasiaa Queens ya Iringa.