DAR ES SALAAM; Wadau wa sekta ya muziki wameiomba serikali kuingiza elimu ya muziki katika mtaala wa shule za msingi, wakisema hatua hiyo itasaidia kugundua na kukuza vipaji vya watoto mapema na kuwaandaa kutumia muziki kama taaluma na chanzo cha ajira.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa kinanda kipya cha Yamaha PSR-SX620 Dar es Salaam, wadau hao walisema Tanzania ina vipaji vingi vya muziki vinavyohitaji kutambuliwa na kulelewa kupitia mfumo rasmi wa elimu.
Msimamizi wa Mauzo wa Yamaha Afrika, Moses Mbogo, alisema elimu hiyo itawasaidia watoto kutambua uwezo wao mapema na kupata ujuzi wa kuendeleza vipaji hivyo.
“Tunazungumzia fursa nyingi zilizopo kwenye sekta ya muziki. Tanzania ina muziki ambao unauza, hivyo vijana wakitumia vizuri fursa hizi wanaweza kufika mbali,” alisema.
Mbogo alisema muziki haupaswi kuangaliwa kama burudani pekee, bali taaluma inayoweza kutoa ajira na fursa za kujiajiri katika maeneo mbalimbali, ikiwamo uimbaji, utunzi, upigaji wa ala, utayarishaji na uhandisi wa sauti.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Topshop Music Limited, Aminmohamed Janmohamed, alisema Tanzania inahitaji kuongeza weledi katika sekta hiyo na kuwajengea watoto msingi wa muziki tangu wakiwa shuleni.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shifaa Pan African Hospitals Limited, Bashir Haroon, alisema utambuzi wa vipaji unapaswa kuanza utotoni badala ya kusubiri hadi vijana wafikie umri mkubwa.
“Mtoto akipewa nafasi mapema ya kujifunza muziki na kuonesha uwezo wake, tunaweza kugundua kipaji chake na kukilea vizuri,” alisema.
Alisema kuingizwa kwa elimu ya muziki katika shule za msingi kunaweza kuwa sehemu ya juhudi za kukuza sekta ya ubunifu na kuwaandaa vijana kutumia vipaji vyao kama rasilimali ya kiuchumi.
Waomba muziki uingizwe kwenye mtaala kukuza vipaji, ajira
DAR ES SALAAM; Wadau wa sekta ya muziki wameiomba serikali kuingiza elimu ya muziki katika mtaala wa shule za msingi, wakisema hatua hiyo itasaidia kugundua na kukuza vipaji vya watoto mapema na kuwaandaa kutumia muziki kama taaluma na chanzo cha ajira. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa kinanda kipya cha Yamaha PSR-SX620 Dar…

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
EntertainmentSherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo. Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria. Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria. Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa. Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao. Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe. Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja. Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja. Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja. Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza. Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.
EntertainmentVP agrees to become basketball patron, names Alikiba, Harmonize as influential figures
DAR ES SALAAM: VICE President Deogratius Ndejembi, has agreed to become the patron of basketball in the country, expressing his passion for the sport and his ambition to see it achieve popularity comparable to football. He urged artists and businesspeople to invest in basketball by owning teams, saying greater private investment would increase competition and…
EntertainmentTJ Vybez expands creative footprint with cinematic visual for ‘YAWA’
By Benjamin Njoku Rising Afrosounds star TJ Vybez is steadily carving out his own lane in Nigeria’s competitive music scene with a sound built on confidence, relatable storytelling and contemporary African rhythms. The singer, who has to his credit songs like ‘Illegal”, “Myself”, “Available” and ‘Baddie” from his EP “I Must Succeed” is expanding his […]
EntertainmentA saint has joined the angels – Tope Alabi mourns Toluwanisings
Nigerian gospel singer Tope Alabi has expressed sadness over the passing of gospel artiste Olayemi Bolaji, popularly known as Toluwanisings, who died at age 41.