Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) inayo furaha kutangaza kuwa Zanzibar itakuwamwenyeji wa Tuzo za Muziki za Trace 2025, tukio kubwalitakalodhaminiwa na kinywaji cha Johnnie Walker kamamdhamini mkuu. Tukio hili linalotarajiwa kufanyika kuanziatarehe 24 hadi 26 mwezi Februari katika hoteli ya kifahari yaMora Resort, visiwani Zanzibar nchini Tanzania, linalengakusherehekea mabadiliko ya muziki na utamaduni wa Kiafrika—sehemu muhimu ya urithi wa kisanaa wa Tanzania na faidayake inayoongezeka kimataifa.  

Tuzo za Trace na Mkutano wa 2025 utatambua vipaji vyamuziki wa Afrika katika vipengele 24 tofauti, ambapo Johnnie Walker itadhamini tuzo mbili kuu: Wimbo Bora wa Mwaka naMsanii Bora Chipukizi. Tukio hili pia litajumuisha mkutanowa siku mbili ambao utakuwa na mijadala ya kibunifu, mafunzo, na majadiliano kuhusu maendeleo ya tasnia ya muziki, teknolojia, na uimarishaji wa chapa barani Afrika. Washirikiwatajumuisha wasanii, mameneja, ma-DJ, maprodyuza, nawadau wengine wa sekta hii kutoka ndani na nje ya Afrika.  
Mwaka huu, ushirikiano huu kati ya Johnnie Walker na Tuzo za Muziki za Trace unasisitiza dhamira ya Johnnie Walker yakusherehekea utamaduni wa Kiafrika na kuchochea mijadalayenye tija. Kama moja ya majukwaa yanayoheshimika zaidi kwamuziki wa Kiafrika na Afro-urban, Tuzo za Trace zinatambuavipaji na uvumbuzi kwa kiwango cha kimataifa, zikitangulizaubunifu, utamaduni, na maendeleo— zikiakisi kaulimbiu yaJohnnie Walker ya ‘Keep Walking’, ambayo inahamasishamaendeleo, ubunifu, na kwenda mbali zaidi.  

Akizungumzia ushirikiano huu, Henry Esiaba, Mkurugenzi waMasoko na Ubunifu wa SBL, alisisitiza umuhimu wa tukio hilikwa Tanzania na chapa ya Johnnie Walker akisema, “Tunajivunia kuwa na Johnnie Walker kama mdhamini mkuu waTuzo za Muziki za Trace 2025 na kuona Tanzania ikiandaa tukiohili linalotambulika kimataifa. Ushirikiano huu hauitangazi tuTanzania kimataifa bali pia inaashiria kaulimbiu ya ‘Keep Walking’–kuadhimisha maendeleo na kuhamasisha vizazivijavyo.”
Naye, Irene Mutiganzi, Mkuu wa Kitengo cha Vinywaji Vikali-Masoko kutoka SBL alisema, “Tuzo za Muziki za Trace 2025 nizaidi ya sherehe ya muziki—ni sherehe ya maendeleo, ubunifu, na uthubutu. Kwa Johnnie Walker, ushirikiano huu ni isharakubwa ya dhamira yetu ya kuwa bega kwa bega na wabunifu nawavumbuzi wanaotengeneza mustakabali wa kesho. Tunatazamia kuonesha ubora wa muziki na utamaduni waKiafrika kwa ulimwengu mzima.”

Katika kipindi cha kuelekea kwenye tukio hili, sehemu nyinginemuhimu ya hafla hii itakuwa Ziara ya Tuzo za Trace, ambayoitatembelea miji mikubwa ya Afrika, ikiwemo Tanzania. Ziara hii itajumuisha maonesho ya moja kwa moja ya muziki na fursaza mashabiki kukutana na wasanii walioteuliwa. Kwa Tanzania, tukio hili litafanyika tarehe 7 mwezi Februari 2025 na litakuwautangulizi wa tukio kuu la utoaji wa tuzo.

Kama mwenyeji, Tanzania itang’ara kama kitovu cha ubunifu, utamaduni, na ukarimu. Zanzibar, yenye mandhari ya kuvutia naurithi wake mkubwa, inatoa mazingira bora kwa tuzo hizi. Ushirikiano huu pia unathibitisha dhamira ya SBL ya kusaidiamipango inayoinua hadhi ya taifa na kusherehekea utajiri wake wa kitamaduni.

Kupitia ushirikiano huu, Johnnie Walker na Trace wataandaaburudani kubwa na ya kipekee wakati wa Tuzo za Trace, ikiwapa wageni burudani inayoendana na chapa ya Johnnie Walker huku wakisherehekea mvuto wa utamaduni wa Afrika.
The post Tuzo za Trace Muziki 2025 zitafanyika Zanzibar first appeared on Millard Ayo.