DAR-ES-SALAAM : MSANII nyota wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Soud maarufu kama Zuchu, ameibua mjadala mkali mitandaoni kufuatia kuachia kwa wimbo wake mpya Amanda, huku akiwajibu vikali mashabiki wanaokosoa mabadiliko ya mwelekeo wake wa kimuziki.
Wimbo huo, uliotayarishwa na S2kizzy, umetolewa katika matoleo mawili clean na explicit na kuwasilisha ladha ya kipekee ambayo imewachanganya baadhi ya mashabiki waliokuwa wakiitegemea sauti ya Bongo Fleva.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu alitoa tamko kali kwa wanaoonesha kutoridhika na kazi yake hiyo mpya, akieleza kuwa yuko huru kubadilika kisanii kadri anavyotaka, bila kulazimika kurudi nyuma ili kumridhisha kila shabiki. “This is the new me. I will be as versatile as I want to be. Na kama unahisi mabadiliko haya hayakufai, nakushauri uniache tu sasa,” aliandika Zuchu kwa msisitizo.
Kauli hiyo imekuja baada ya baadhi ya mashabiki kueleza kutopendezwa na mtindo mpya wa wimbo huo, wakidai kuwa umetoka nje ya msingi wa Bongo Fleva waliomzoea.Hata hivyo, Zuchu amesisitiza kuwa huu ni wakati wa wasanii kuvuka mipaka ya kawaida na kuonesha ubunifu zaidi katika muziki. “Nimechoka kuimba vitu vile vile kila siku… Kama unapenda msanii kwa vigezo vya Grammy, feel free kushabikia mwingine,” aliandika.
Zuchu pia hakusahau kuwashukuru mashabiki waliomuunga mkono katika hatua hii mpya, akitoa ujumbe wa matumaini: “I love you. Funga mkanda, maana safari ndo kwanza imeanza.” SOMA: Zuchu ahoji ugawaji tuzo za TMA
Wimbo wa Amanda sasa umeibua mjadala mkubwa: Je, huu ni mwanzo wa hatua ya kimataifa kwa Zuchu, au ni kupotea kwenye misingi ya Bongo Fleva?
“This is the New Me!” Zuchu awajibu wakosoaji

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
EntertainmentSherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo. Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria. Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria. Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa. Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao. Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe. Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja. Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja. Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja. Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza. Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.
EntertainmentVP agrees to become basketball patron, names Alikiba, Harmonize as influential figures
DAR ES SALAAM: VICE President Deogratius Ndejembi, has agreed to become the patron of basketball in the country, expressing his passion for the sport and his ambition to see it achieve popularity comparable to football. He urged artists and businesspeople to invest in basketball by owning teams, saying greater private investment would increase competition and…
EntertainmentTJ Vybez expands creative footprint with cinematic visual for ‘YAWA’
By Benjamin Njoku Rising Afrosounds star TJ Vybez is steadily carving out his own lane in Nigeria’s competitive music scene with a sound built on confidence, relatable storytelling and contemporary African rhythms. The singer, who has to his credit songs like ‘Illegal”, “Myself”, “Available” and ‘Baddie” from his EP “I Must Succeed” is expanding his […]
EntertainmentA saint has joined the angels – Tope Alabi mourns Toluwanisings
Nigerian gospel singer Tope Alabi has expressed sadness over the passing of gospel artiste Olayemi Bolaji, popularly known as Toluwanisings, who died at age 41.