Tasima kutoa mafunzo kwa wasanii wa singeli
CHAMA cha Muziki wa Singeli Tanzania (TASIMA) kinatarajiwa kuwajengea uwezo wasanii wa muziki huo na kuufanya kuwa muziki…
The post Tasima kutoa mafunzo kwa wasanii wa singeli appeared first on HabariLeo.
CHAMA cha Muziki wa Singeli Tanzania (TASIMA) kinatarajiwa kuwajengea uwezo wasanii wa muziki huo na kuufanya kuwa muziki wakipekee zaidi itakaotikisa anga za kimataifa
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja Masudi Kandoro ‘Kandoro Baba’ amesema kuwa kupitia Kauli aliyosema Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Palamagamba Kabudi kuwa Muziki wa Singeli unatakiwa kupewa kipaumbele.
“Tunaunga Mkono kauli hizo tofauti za viongozi waoutazamia muziki wa Singeli na kuona kuwa ni muziki utakao tubadilisha na kututangaza zaidi kimataifa.
“Lengo kuwabadilisha wasanii kuwa na matendo mazuri, muonekano pamoja na kuwapatia elimu itakayowapo uwelewa wa wao kujua vitu ikiwemo na kujifunza lugha za watu wengine zitakazowafanya kuwasiliana vizuri na mashabiki wao.
Aidha ameongeza kuwa kumekuwa na wasanii tofauti tofauti wa Kimataifa ambao wamekuwa wakioonyesha kufurahia na mziki wa singeli.
“Niwakati wa wasanii kuungana na kututangaza muziki wa pekee utakaopeperudha bendera na kutuletea tuzo za Grammy kwa upekee wake.
“Wasanii kama Snop Dog, Chris Brown wamekuwa wakisapoti muziki wa Singeli kwa kuimba muziki huo, ambao ukizingatia unaweza kutuletea tuzo ya grammy nchini ni muziki wa Singeli.”amesema Kandoro
“Singeli to the World tuta hakikisha wasanii wanajikita kutangaza vitu vya Kitanzania zaidi kwa kuwashirikisha wasanii mbalimbali kama wabunifu wa ndani pamoja na wachoraji ili kutengeneza kitu kizuri.
Kwa upande wake Samadu abdallah, ‘Samio love’ amesema kuwa Muziki wa Singeli na kuimba matusi ni jambo la mtu binafsi ili muziki wako ueshimike unapaswa kuwa na maadili.
“Aina ya muziki wa Singeli kuimba matusi sio chama bali ni mtu binafsi na kile anachokiimba yeye binafsi itakuwa nafasi ya kutenganisha matusi na kuburudishaji katika kuimba Singeli.
The post Tasima kutoa mafunzo kwa wasanii wa singeli appeared first on HabariLeo.