Video
TANROADS YAFAFANUA UJENZI DARAJA LA MAKONTENA ILEJE
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
#HABARI: Uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe umetoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa daraja la makontena lililopo katika Mto Kalembo, Kijiji cha Ibungu wilayani Ileje linalounganisha zaidi ya kata nne, ukieleza kuwa daraja hilo si la kudumu. Ufafanuzi huo umetolewa na Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Songwe, Mhandisi Silvan Mloka, kufuatia hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Wilman Ndile, kufika eneo hilo, kuonesha hofu ya makontena hayo kusombwa na maji, na kuagiza wakala huo kufanya tathmini. Akifafanua zaidi, Mhandisi Mloka amesema daraja hilo la muda limejengwa kama njia ya dharura baada ya daraja la awali kuondolewa ili kupisha ujenzi wa daraja la kudumu. Ameongeza kuwa makontena hayo yamewekwa katika kipindi hiki cha ujenzi ili kuhakikisha barabara hiyo inaendelea kupitika na huduma za usafiri hazisimami kwa wananchi. RADIO ZETU KWENYE VING’AMUZI: Radio One: Azam 061, Digitek 110, Capital Radio: Azam 383, Digitek 112, Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Mix by Yas, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania Follow @itvtz @radioonetanzania @itv2tanzania
Related stories
GeneralNavy intercepts 89,000 litres of stolen crude, illegal diesel in Rivers
By Kingsley Omonobi The Nigerian Navy has intercepted about 35,000 litres of suspected stolen crude oil and uncovered an illegal refining site containing an additional 54,000 litres of suspected illegally refined Automotive Gas Oil (AGO) in Rivers State. The operation, conducted on November 22 by personnel of Nigerian Navy Ship (NNS) Pathfinder around Okarki Creek […]
GeneralNovember 23, 2026
GeneralDr David Nelson Okello takes the helm of Uganda Veterinary Association
Arua, Uganda | THE INDEPENDENT | The Uganda Veterinary Association (UVA) has elected a new leader who is bringing a “Green Agenda” with him. At the association’s Annual General Meeting (AGM) held at Hotel le Confidentiale in Arua City on November 20, 2026, Dr David Nelson Okello was elected President for the 2026–2028 term by…
General