MSANII wa Bongo, Diamond Platnumz, amevunja kimya chake kufuatia hatua yake ya kutotumbuiza katika tamasha la Furaha City Festival jijini Nairobi.
Msanii huyo inasemekana alipokea kitita cha dola 150,000 (takriban Sh19.3 milioni) ili kupamba hafla hiyo lakini akaondoka ukumbini bila kutumbuiza, na ameweka wazi kuwa hatarejesha donge hilo.
Katika video iliyoelekezwa kwa mashabiki wake, Diamond anaeleza kuwa yeye hufuata kikamilifu sera zake za utendakazi, ikiwa ni pamoja na kuheshimu muda uliopangwa.
“Siwezi kulipwa dola 150,000 kisha nije kupigana kutumbuiza jukwaani,” alisema.
“Nitafika ukumbini kwa wakati kusubiri mwandalizi wa hafla aniite jukwaani, nitaendelea kuangalia saa yangu, na muda wangu wa kutumbuiza ukiisha nitatoka nje ya ukumbi huo na sirudishi pesa zozote."
Diamond alisisitiza kuwa hajihusishi na mabishano na wasanii wengine au waandalizi ili kupata nafasi yake jukwaani.
"Sihitaji kujadiliana na waandalizi au kupigana na wasanii wengine ili niruhusiwe kutumbuiza. Hiyo sio nidhamu yangu," alisema kwenye video hiyo.
Mwimbaji huyo pia alizungumzia madai yaliyotolewa na msanii wa Kenya Willy Paul, ambaye anadai kuwa uongozi wa Diamond ulimzuia kutumbuiza ili kuruhusu nyota huyo wa Tanzania kupanda jukwaani kwanza.
"Itakuwa upumbavu kwangu kufanya hivyo; ina maana gani?" Diamond alihoji.
"Mimi ndiye mhusika mkuu, ambayo ina maana wasanii wengine wote wanaigiza kabla yangu. Willy Paul anajaribu tu kutengeneza drama kwa sababu bado anatafuta umaarufu. Huu ni upuuzi—muziki unahitaji bidii na usimamizi mzuri, si ushupavu na huruma."
Alisema kuwa alifika mapema na kusubiri kwenye gari lake, kwani anapendelea kutokaa nyuma ya jukwaa.
“Tangu nilipofika kulitokea fujo ambazo hazikuisha, meneja wangu alimpigia simu mratibu kumuuliza kwa nini kuna fujo nyingi na kwanini mambo hayakusimamiwa ipasavyo, alijibu na kusema alihitaji dakika 10 zaidi. Kwa bahati mbaya, ghasia zilfika mahali nilipoketi," Diamond anaelezea.
Hali ilipozidi kudorora, meneja wa Diamond aliamua ni bora amrudishe hotelini kwake.
"Kulikuwa na fujo pande zote za hafla, na sielewi kwa nini ilifanyika," anasema.
"Msanii hawezi kutumbuiza chini ya hali kama hizi, na wengine wanaweza kuiona kama kukosa heshima."
Diamond anasema alisubiri kwa takribani saa tatu bila kupanda jukwaani, akieleza kusikitishwa kwake lakini akathibitisha kuwa hakuwa na la kufanya.
Wakati huo huo waandalizi wa tamasha wamejitetea.
“Tunasikitika sana kutangaza kuwa Diamond Platnumz hakutumbuiza katika tamasha la Furaha City kama ilivyopangwa, sisi tukiwa waandalizi tulijitahidi yeye na timu yake walikuwa sawa, kuhakikisha mipango na dharura zote zilishughulikiwa ili kusiwe na matatizo.. Hata hivyo tabia na matakwa ya timu yake yalionekana kuwa ya kusikitisha na ya kupindukia kupita kiasi," ilisema taarifa hiyo.
Huku wakikiri kulitokea suala dogo la kiusalama linalomhusisha msanii mwingine, walifafanua, "Tulitatua kwa haraka na kuhakikisha kwamba tamasha iliendelea kwa njia salama na ya kitaaluma. Tunaamini katika kuwatendea wasanii wote usawa na kudumisha viwango vya ubora wa juu kwa kila mtu anayehusika."
IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
Sirudishi hata senti, Diamond aapa licha ya kutotumbuiza tamasha la Furaha City
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EntertainmentSherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo. Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria. Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria. Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa. Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao. Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe. Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja. Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja. Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja. Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza. Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.
EntertainmentVP agrees to become basketball patron, names Alikiba, Harmonize as influential figures
DAR ES SALAAM: VICE President Deogratius Ndejembi, has agreed to become the patron of basketball in the country, expressing his passion for the sport and his ambition to see it achieve popularity comparable to football. He urged artists and businesspeople to invest in basketball by owning teams, saying greater private investment would increase competition and…
EntertainmentTJ Vybez expands creative footprint with cinematic visual for ‘YAWA’
By Benjamin Njoku Rising Afrosounds star TJ Vybez is steadily carving out his own lane in Nigeria’s competitive music scene with a sound built on confidence, relatable storytelling and contemporary African rhythms. The singer, who has to his credit songs like ‘Illegal”, “Myself”, “Available” and ‘Baddie” from his EP “I Must Succeed” is expanding his […]
EntertainmentA saint has joined the angels – Tope Alabi mourns Toluwanisings
Nigerian gospel singer Tope Alabi has expressed sadness over the passing of gospel artiste Olayemi Bolaji, popularly known as Toluwanisings, who died at age 41.