KAMPUNI inayojihusisha na ubunifu wa kidijitali, Wave 360 Africa, imetambuliwa na serikali kwa mchango wake katika kukuza sekta ya ubunifu nchini.
Kampuni hiyo ilipokea utambuzi huo wakati wa Maonyesho ya Kimataifa Nairobi yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Nairobi.
Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe, aliipongeza kampuni hiyo akisema kazi ya kampuni za vijana katika sekta ya ubunifu inaonyesha namna teknolojia inavyoweza kutumiwa kufikisha ujumbe kwa umma.
Kagwe alisema vijana nchini wana uwezo wa kutumia ubunifu na teknolojia kuunda nafasi za ajira na kusaidia kukuza biashara.
“Tunapaswa kuendelea kuunga mkono biashara kama hizi kwa sababu zinaunda nafasi, zinaongoza mijadala na kuonyesha kile ambacho vipaji vya Kenya vinaweza kufanya,” alisema Kagwe.
Maonyesho hayo, yaliyoanza Septemba 28 na kukamilika Oktoba 4, yaliwaleta pamoja washiriki kutoka sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, biashara, viwanda, teknolojia na elimu.
Wave 360 Africa ilianzishwa mwaka 2022 na inajihusisha na kampeni za kidijitali, utangazaji, matukio na shughuli nyingine za ubunifu zinazolenga kuunganisha biashara na wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Zedekiah Mukoya, alisema kutambuliwa kwao ni motisha kwa vijana wanaojaribu kujenga biashara katika sekta ya ubunifu.
Alisema kampuni hiyo inalenga kutumia uelewa wa utamaduni na mienendo ya Wakenya katika kuunda ujumbe unaoeleweka kwa wananchi.
Kwa Wakenya wengi, hasa vijana wanaotumia mitandao ya kijamii kila siku, kampuni za aina hiyo zimekuwa sehemu muhimu ya namna mashirika yanavyowasiliana na umma kupitia simu na majukwaa ya kidijitali.
Utambuzi huo wa mwaka huu unafuatia tukio la mwaka jana ambapo Rais William Ruto alitembelea kampuni hiyo ya Wave 360 wakati wa maonyesho hayo.
Kampuni hiyo pia imepanua shughuli zake nje ya Kenya, baada ya kuingia Uganda mwaka 2025.
Kwa kampuni hiyo iliyoanzishwa miaka minne iliyopita, utambuzi huo unaongeza orodha ya hatua katika safari yake ya kujenga nafasi katika sekta ya ubunifu Afrik
a Mashariki.
Serikali yatambua kampuni inayowainua vijana kibiashara

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessWafanyabiashara Moro wahamasishwa malipo kidigitali
MOROGORO:BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewahimiza wafanyabiashara nchini kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali katika manunuzi na mauzo ya bidhaa zao, ikieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya mzunguko wa fedha katika uchumi na kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na kubeba fedha taslimu. Rai hiyo imetolewa na Ofisa wa BOT kutoka Kurugenzi ya Mifumo…
BusinessWhy Ajaokuta remains moribund after 40 years — NES president
By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The President of the Nigerian Economic Society (NES), Dr. Baba Musa, has attributed the continued failure of the multi-billion-dollar Ajaokuta Steel Company to the absence of sustained long-term development plans. Musa said this at the 2026 National Growth and Development Forum (NGDF), with the theme, “The Nigeria We Want: […]
BusinessBoT yaimarisha ujumuishi wa kifedha kwa walemavu
IRINGA: Walemavu mkoani Iringa wameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa elimu ya fedha inayowasaidia kuelewa utunzaji sahihi wa fedha, matumizi ya mikopo na namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti, huku wakiiomba benki hiyo kupanua wigo wa mafunzo hayo ili yawafikie walemavu wengi zaidi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini. Pongezi hizo…
BusinessMuseveni, Samia push railway link to DRC
This could reshape trade routes into the Great Lakes region.