Mwimbaji nguli wa Muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, Rose Mhando amesema amekiri kwamba Mkurugenzi wa Msama Promotions ambaye ni mwandaaji wa matamasha mbalimbali ya Muziki wa Injili Alex Msama, ni zaidi ya Baba kwake kwani tangu alipoanza kazi zake za Uimbaji wa nyimbo za Injili amekuwa akifanya naye kazi kwa wema bila dhuluma na Msama hajawahi nidhulumu.
Muhando alisema yeye pamoja na baadhi ya wasanii wenzake wa muziki wa Injili, hawawezi kujivunia mafanikio yao bila kutaja jina la Alex Msama ambaye hivi karibuni alipata tuzo ya Muandaaji Bora wa Muziki wa Injili wa wakati wote
Rose ametoa kauli hiyo baada ya hivi karibuni kuwapo taarifa kwenye mitandao ya kijamii, zikidai msanii huyo aliwahi kudhulumiwa haki zake na Msama.
Akizungumzia kuhusu madai hayo, Rose alisema ameshitushwa sana na kusikitishwa sana na tarifa hizo na kuongeza kuwa hajui zimetokea wapi na watunzi wa uzushi huo wana lengo gani.
Alisema katika maisha yake mafanikio yake ya muziki huo, Malkia huyo wa Muziki wa Injili alisema hawezi kumsahau na kutaja jina la Msama ambaye ametumia muda mwingi wa maisha yake na fedha zake kuibua na kukuza na kulea vipaji wa vya muziki wa Injili na kuhakikisha haki zao zinalindwa.
Akitolea mfano, Rose anasema Msama alikuwa ananisaidia kutoa ushauri wakati wa kuandaa muziki, alitoa msaada mkubwa wa fedha kuingia studio na kurekodi na zaidi ya yote alianzisha vita ya kukabiliana na wahuni waliokuwa wakiiba na wakiuza cd zetu na kuwafanya wasanii hao kukosa haki zao na kuishi maisha ya shida.
“Kwangu mimi, Msama ni zaidi ya Baba, amenisaidia mambo mengi sana, kuanzia fedha hadi ushauri, amenivumilia hata ninapomkwaza , leo mtu anaweza kuchapisha taarifa na kueleza kwamba eti Msama aliwahi kunidhulumu, hii sio kweli kabisa sjawahi na siwezi kusema kauli hiyo dhidi ya Msama, alisisitiza Rose Muhando.
Alisema kuwa “yapo mambo madogo ya kibinadamu yaliyowahi kutokea wakati wa kazi, ikiwamo mimi mwenyewe kumkwaza Msama, lakini hiyo haina maana kwamba Msama amewahi kunidhulumu haki zangu
Kwa mujibu wa Rose, ataendelea kufanya kazi na Msama wakati wowote atakapohitajika na ataendelea kuwa chini yake kwani anaamini mfanyabiashara huyo anamapezi ya dhati ya muziki wa Injili toka moyoni na Serikali inapaswa kumuangalia kwa jicho tofauti na hata kumpa msaada.
” Mimi na baadhi ya wasanii wenzangu tulifika hatua ya kumuita Msama kuwa ni Askofu wa Muziki wa Injili, yule Baba ana mapenzi na muziki wa Injili toka moyoni, ni mtumishi wa Mungu aliyeamua kufanya utumishi wake kwa kukuza vipaji vya wasanii wa muziki huo.
Alimwomba Mh Rais Samia Suluhu Hassan kumuangalia Msama na kumlinda pale anaponyanyaswa na baadhi ya watendaji wa Serikali kwani kumuua Msama ni kuuwa ndoto na maisha ya wasanii wa Muziki wa Injili.
Kuhusu hatma yake kwenye muziki huo, Rose alisema muda mrefu alijiweka kando kutokana na changamoto za kiafya, lakini hivi sasa anaandaa Albamu mpya ya muziki wake ambayo itazinduliwa wakati wowote mwaka huu.
“Baada ya kutoka hospitali, nilijipa muda wa kupumzika, lakini hivi sasa naandaa Albamu yangu ya kukata na shoka, itazinduliwa wakati wowote mwaka huu na itakapokuwa tayari nitawajulisha washabiki wangu,”
The post Rose Mhando: Msama ni baba kwangu acheni kunigombanisha nae first appeared on Millard Ayo.
Rose Mhando: Msama ni baba kwangu acheni kunigombanisha nae
This story was originally published by Milard Ayo.
Read the full story at Milard AyoRelated stories
EntertainmentSherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo. Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria. Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria. Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa. Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao. Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe. Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja. Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja. Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja. Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza. Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.
EntertainmentVP agrees to become basketball patron, names Alikiba, Harmonize as influential figures
DAR ES SALAAM: VICE President Deogratius Ndejembi, has agreed to become the patron of basketball in the country, expressing his passion for the sport and his ambition to see it achieve popularity comparable to football. He urged artists and businesspeople to invest in basketball by owning teams, saying greater private investment would increase competition and…
EntertainmentTJ Vybez expands creative footprint with cinematic visual for ‘YAWA’
By Benjamin Njoku Rising Afrosounds star TJ Vybez is steadily carving out his own lane in Nigeria’s competitive music scene with a sound built on confidence, relatable storytelling and contemporary African rhythms. The singer, who has to his credit songs like ‘Illegal”, “Myself”, “Available” and ‘Baddie” from his EP “I Must Succeed” is expanding his […]
EntertainmentA saint has joined the angels – Tope Alabi mourns Toluwanisings
Nigerian gospel singer Tope Alabi has expressed sadness over the passing of gospel artiste Olayemi Bolaji, popularly known as Toluwanisings, who died at age 41.