ZAIDI ya wakulima 700,000 wa majanichai wanatarajiwa kupokea malipo ya bonasi ya kila mwaka leo, huku fedha hizo zikiingia katika akaunti zao pamoja na malipo ya kawaida ya mwezi Septemba.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kilimo cha Majanichai (KTDA) Enos Njeru, alisema fedha hizo zilitolewa Ijumaa kwa hivyo wakulima watazipokea kwenye benki leo.
Katika mabadiliko ya utaratibu wa kawaida, viwanda vya chai ndivyo vitakavyotangaza viwango vya bonasi, vinavyojulikana pia kama malipo ya pili, badala ya bodi ya KTDA kufanya hivyo kwa niaba yao.
Jumla ya fedha zitakazolipwa na viwanda 77 vilivyounganishwa kuwa vitengo 54 bado hazijatangazwa.
Katika mwaka wa kifedha wa 2024/2025, wakulima walipokea Sh69.8 bilioni, ambazo ni Sh20 bilioni chini ya Sh89.6 bilioni zilizolipwa mnamo 2023/2024.
Ingawa viwango rasmi vya mwaka huu havijatangazwa, bonasi zinakadiriwa kuwa kati ya Sh12.50 na Sh50 kwa kila kilo ya majanichai mabichi, kutegemea kiwanda husika.
Mwenyekiti wa Kiwanda cha Chai cha Tirgaga, Kipngeno Rono, alisema viwanda huzingatia gharama za uendeshaji na bei ya chai sokoni kuamua malipo kwa wakulima.
Gharama za umeme, kuni, mafuta, maji, ukusanyaji wa majani, gharama ya kutengeneza mashine, mishahara na mikopo pia huzingatiwa.
Malipo hayo hutegemea mwaka wa kifedha unaoisha Juni 30. Bei za mnada wa chai Mombasa na thamani ya Shilingi dhidi ya Dola pia huathiri bonasi.
Raha wakuzaji majani-chai wakiendea bonasi ‘nzuri’ leo

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessWafanyabiashara Moro wahamasishwa malipo kidigitali
MOROGORO:BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewahimiza wafanyabiashara nchini kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali katika manunuzi na mauzo ya bidhaa zao, ikieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya mzunguko wa fedha katika uchumi na kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na kubeba fedha taslimu. Rai hiyo imetolewa na Ofisa wa BOT kutoka Kurugenzi ya Mifumo…
BusinessWhy Ajaokuta remains moribund after 40 years — NES president
By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The President of the Nigerian Economic Society (NES), Dr. Baba Musa, has attributed the continued failure of the multi-billion-dollar Ajaokuta Steel Company to the absence of sustained long-term development plans. Musa said this at the 2026 National Growth and Development Forum (NGDF), with the theme, “The Nigeria We Want: […]
BusinessBoT yaimarisha ujumuishi wa kifedha kwa walemavu
IRINGA: Walemavu mkoani Iringa wameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa elimu ya fedha inayowasaidia kuelewa utunzaji sahihi wa fedha, matumizi ya mikopo na namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti, huku wakiiomba benki hiyo kupanua wigo wa mafunzo hayo ili yawafikie walemavu wengi zaidi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini. Pongezi hizo…
BusinessMuseveni, Samia push railway link to DRC
This could reshape trade routes into the Great Lakes region.