DAR ES SALAAM: Makamu wa Rais wa wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amekubali kuwa mlezi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, akieleza kuwa anaupenda mchezo huo na kutamani kuuona ukipata umaarufu mkubwa kama ilivyo soka.
Aidha, amewataka wasanii na wafanyabiashara nchini kuwekeza katika mchezo huo kwa kumiliki timu ili kuupa msisimko wa kuongeza ushindani kama ilivyo kwa soka, huku akiwataja wasanii kama Ali Kiba na Harmonize kuwa miongoni mwa wanaoweza kutumia uishawishi wao kuendeleza mchezo kama alivyofanya Emanuel Mkono ‘Nahreel’ kwa timu ya Reel.
Ndejembi alitoa kauli hiyo wakati wa fainali za Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kati ya Dar City dhidi ya Stein Warriors zilizofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa IST, Masaki, akisema anaamini mpira wa kikapu unaweza kuvutia mashabiki wengi zaidi endapo wadau wataungana kuwekeza katika mchezo huo.
Amesema moja ya mambo yaliyomvutia katika mashindano hayo ni ushiriki wa timu za wanawake, akibainisha kuwa uwepo wa timu 17 za wanawake unaonesha kuongezeka kwa mwamko wa mchezo huo miongoni mwa wanawake.
Amesema ili kufikia lengo hilo, kunahitajika wadhamini zaidi, wafanyabiashara na wasanii kujitokeza kuwekeza katika timu za mpira wa kikapu, akitoa mfano wa namna uwekezaji unavyoweza kusaidia timu kukua na kufanya vizuri katika mashindano.
Alitaja mfano wa timu ya wanawake ya Reel, ambayo amesema imepata mafanikio baada ya kupata wadau wanaoiunga mkono, akisisitiza kuwa ushirikiano wa wadau unaweza kuleta mabadiliko katika mchezo huo.
Kuhusu miundombinu, Ndejembi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, itafanya juhudi kuhakikisha mahitaji ya viwanja vya kisasa vya mpira wa kikapu yanapatiwa ufumbuzi.
Pia, ameishukuru menejimenti ya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) kwa kutoa uwanja kwa ajili ya fainali hizo, akisema hatua hiyo ni mchango muhimu katika kuendeleza mchezo wa mpira wa kikapu nchini.
Ndejembi akubali kuwa mlezi wa mpira wa kikapu

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
BusinessWafanyabiashara Moro wahamasishwa malipo kidigitali
MOROGORO:BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewahimiza wafanyabiashara nchini kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali katika manunuzi na mauzo ya bidhaa zao, ikieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya mzunguko wa fedha katika uchumi na kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na kubeba fedha taslimu. Rai hiyo imetolewa na Ofisa wa BOT kutoka Kurugenzi ya Mifumo…
BusinessWhy Ajaokuta remains moribund after 40 years — NES president
By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The President of the Nigerian Economic Society (NES), Dr. Baba Musa, has attributed the continued failure of the multi-billion-dollar Ajaokuta Steel Company to the absence of sustained long-term development plans. Musa said this at the 2026 National Growth and Development Forum (NGDF), with the theme, “The Nigeria We Want: […]
BusinessBoT yaimarisha ujumuishi wa kifedha kwa walemavu
IRINGA: Walemavu mkoani Iringa wameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa elimu ya fedha inayowasaidia kuelewa utunzaji sahihi wa fedha, matumizi ya mikopo na namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti, huku wakiiomba benki hiyo kupanua wigo wa mafunzo hayo ili yawafikie walemavu wengi zaidi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini. Pongezi hizo…
BusinessMuseveni, Samia push railway link to DRC
This could reshape trade routes into the Great Lakes region.