MWIMBAJI Marco Joseph wa Kundi la Waimbaji la Zabron kutoka Tanzania, linakojulikana kwa nyimbo zao maarufu za Kiswahili, ukiwemo uliovuma katika kampeni ya Rais William Ruto 2022, amefariki.
Alifariki dunia Agosti 21, 2024, kutokana na ugonjwa wa moyo alipokuwa akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika mahojiano kwa simu na 'Taifa Leo Dijitali,' dadake Marco, Victoria Zabron, alisema kakake alianza kuugua wiki moja iliyopita siku chache kabla ya tamasha waliloshiriki Kisumu.
“Alilazimika kubaki nyuma kutafuta matibabu, madaktari walisema moyo wake ulikuwa na tatizo lililohitaji kufanyiwa upasuaji wa dharura, alikuwa akipatiwa matibabu ya moyo katika Hospitali ya Muhimbili lakini haukufaulu, mazishi yatafanyika Mikocheni, nyumbani kwa shangazi yake. Kwa sasa, mwili bado uko katika mochari," Victoria alisema.
Kulingana na Mwenyekiti wa Kwaya ya Zabron Singers, Japeh Zabron, kaka yake alipatwa na mshtuko wa moyo walipokuwa ziarani Kenya siku chache zilizopita.
Juhudi za kumtibu zilifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, lakini alipewa rufaa ya kwenda JKCI kwa matibabu zaidi kabla ya kufariki dunia akipatiwa matibabu.
Miongoni mwa nyimbo alizotamba nazo akiwa na kundi hilo ni pamoja na “Mkono wake Bwana,” “Swetie Sweetie,” “Sisi Ndio Wale,” “Uko Single,” “Nakutuma Wimbo,” na nyingine nyingi.
Kakake mdogo, Japhet Zabron, pia amemsifu mwimbaji huyo.
"Sikutaka kupost chochote kuhusu hili maana nilikuachia wewe Mungu lakini Mungu sasa umenifanyia hiki hiki. Nooooo hawezi kuwa hivi hapana🙌🏽 Ooh God no." aliandika kwenye mitandao ya kijamii Waimbaji wa Zabron walipata umaarufu kupitia wimbo wao wa 'Mkono Wa Bwana.'
Tangu wakati huo, wamewavutia mashabiki kwa nyimbo nyingine nyingi.
Wanachama wengine wa kwaya hiyo ni pamoja na Victoria Zabron, Jamila Dotto, Samuel Joseph, Semroza Godfrey, Grace Madata na Joyce Zabron.
Katika mahojiano yaliyopita, Japhet, mwalimu wa kikundi alikumbuka jinsi kikundi kiliibuka:
“Tulipokuwa tukisoma sekondari tulienda studio tukarekodi wimbo, hatukuwa na pesa ikabidi tukope kwa watu ili kulipia muda wa studio, ulirekodiwa vibaya hata tukaona aibu kuutoa wimbo huo. Karibu tukate tamaa."
Wimbo wa "Mkono wa Bwana" ulivuma wakati wa kampeni za Rais William Ruto na kupelekea Zabron Singers kutunukiwa heshima ya kutumbuiza katika hafla ya kuapishwa kwake.
Mwimbaji wa Zabron Singers kutoka Tanzania afariki
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EntertainmentSherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo. Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria. Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria. Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa. Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao. Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe. Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja. Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja. Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja. Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza. Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.
EntertainmentVP agrees to become basketball patron, names Alikiba, Harmonize as influential figures
DAR ES SALAAM: VICE President Deogratius Ndejembi, has agreed to become the patron of basketball in the country, expressing his passion for the sport and his ambition to see it achieve popularity comparable to football. He urged artists and businesspeople to invest in basketball by owning teams, saying greater private investment would increase competition and…
EntertainmentTJ Vybez expands creative footprint with cinematic visual for ‘YAWA’
By Benjamin Njoku Rising Afrosounds star TJ Vybez is steadily carving out his own lane in Nigeria’s competitive music scene with a sound built on confidence, relatable storytelling and contemporary African rhythms. The singer, who has to his credit songs like ‘Illegal”, “Myself”, “Available” and ‘Baddie” from his EP “I Must Succeed” is expanding his […]
EntertainmentA saint has joined the angels – Tope Alabi mourns Toluwanisings
Nigerian gospel singer Tope Alabi has expressed sadness over the passing of gospel artiste Olayemi Bolaji, popularly known as Toluwanisings, who died at age 41.