MSHUKIWA ameambia mahakama kwamba hajuti kujihusisha na kilimo cha bangi baada ya kushindwa kupata ajira licha ya kuwa na cheti cha ufundi wa magari.
Bw Geoffrey Lingori, 58 alifikishwa mbele ya Hakimu Mwandamizi Mkuu, Kimani Mukabi katika Mahakama ya Eldoret, akikabiliwa na mashtaka mawili ya kulima na kusafirisha bangi.
Kesi hiyo itatajwa Septemba 18, 2026, kwa maelekezo zaidi.
Alishtakiwa kwa kulima bangi katika shamba la robo ekari kijijini Malel, Kapseret, ambako maafisa walidai kumpata na mimea hiyo yenye uzito wa gramu 34,000 na thamani ya Sh1.032 milioni.
Anakabiliwa pia na shtaka la kusafirisha gramu 50 za bangi zenye thamani ya Sh1,500.
Badala ya kuonyesha majuto, Lingori aliambia mahakama kuwa kilimo hicho ndicho chanzo chake kikuu cha mapato.
“Mheshimiwa Hakimu, ni kweli kwamba mimi hupanda bangi katika kipande changu kidogo cha ardhi kama chanzo changu kikuu cha mapato,” alisema.
Alisema alianza kulima bangi zaidi ya miaka 10 iliyopita baada ya kuhitimu kutoka Rift Valley Technical Training Institute (RVTTI) jijini Eldoret.
Lingori alisema alitafuta ajira akiwa na matumaini ya kujenga taaluma yake, lakini akakumbana na changamoto nyingi ikiwemo kukosa kazi.
Kesi hiyo itatajwa Septemba 18, 2026, kwa maelekezo zaidi.
Mwanamume aambia korti hajuti kukuza bangi baada ya kukosa ajira

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
Jobs and CareerSanwo-Olu gives LASUED best graduate N5m, job
By Elizabeth Osayande Lagos State Governor, Babajide Sanwo-Olu, has rewarded the overall best graduating student of the Lagos State University of Education (LASUED), Blessed Mercy Olawunmi, with N5 million and automatic employment. The award was announced on Thursday, November 19, during the institution’s maiden convocation ceremony held at its Oto/Ijanikin campus. Olawunmi, of the Department […]
Joburg tightens water restrictions as consumers face higher tariffs
Johannesburg residents face Level 2 water restrictions and higher tariffs starting in November and December as the city aims to reduce daily consumption by 200 million litres to ease pressure on the Rand Water supply.
Joburg Council could face interdict over Soweto revote
The People of Joburg party has approached the Gauteng High Court over an irregular recount in Soweto's Ward 31, threatening to interdict the city council's first sitting and stall coalition negotiations.
Jobs and CareerInternship drive faces execution reality check
The government is stepping up efforts to expand employment opportunities for young Tanzanians, with plans to provide 30,000 internship placements while addressing gaps in access to jobs, training and business opportunities.