Video
MENEJA WA SIMBA AWATOLEA UVIVU WACHAMBUZI/ AMTAJA BERNARD MORRISON/AWAJIBU WANAOSEMA MZEE
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
Meneja wa Simba SC, Patrick Rweyemamu, amewakosoa baadhi ya wachambuzi na watu wanaojadili masuala ya soka, akidai kuwa wengi wao hawazingatii uhalisia wa mchezo na taarifa sahihi wanapotoa maoni yao. Rweyemamu amesema kuna watu ambao awali alikuwa akiwaheshimu kutokana na namna walivyokuwa wakichambua masuala ya soka, lakini amebadilisha mtazamo wake kwa sababu amebaini kuwa baadhi yao wamekuwa wakibadilika katika misimamo yao, akiwafananisha na kinyonga. Amesema baadhi ya watu hao leo wanaweza kuzungumza jambo lenye mantiki, lakini siku inayofuata wakatoa kauli ambazo kwa maoni yake hazina msingi. Aidha, Rweyemamu amedai kuwa asilimia 99 ya watu wanaozungumzia soka hawautendei haki mchezo huo, akieleza kuwa wengi hutanguliza maoni binafsi badala ya kuchunguza chanzo cha taarifa na kujikita katika ukweli wa mambo. Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : bit.ly/itvtanzania Facebook : bit.ly/2KeQNl3 Twitter : bit.ly/2XG7aii Instagram : bit.ly/34KItmg
Related stories
GeneralKAGOMA: MIMI HUWA NAJITAHIDI KUFANYA KILE MWALIMU ANANITAKA NIFANYE
GeneralBAADA YA KASHFA YA PENZI LA MCHEPUKO, AREJESHWA KITI CEO NVIDIA
GeneralMRIGO: MGUNDA NI MZEE WANGU NIMEISHI NAE NAMUNGO
GeneralBOSI KASEMA TAREHE 27 ISIGUSWE
BOSI KASEMA TAREHE 27 ISIGUSWE🔥 #breaking #globaltv #nairobi #globaltvonline