Mchumba wa Jux apewa ubalozi wa taulo za kike Ora

Habari Leo
Published: Jan 16, 2025 13:58:42 EAT   |  Entertainment

DAR-ES-SALAAM: MPENZI wa msanii wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’, kutoka nchini Nigeria, Priscilla Ojo, amesema anatamani kuwapatia…

The post Mchumba wa Jux apewa ubalozi wa taulo za kike Ora appeared first on HabariLeo.

DAR-ES-SALAAM: MPENZI wa msanii wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’, kutoka nchini Nigeria, Priscilla Ojo, amesema anatamani kuwapatia zawadi wasanii wa kike hapa nchini, Faustina Mfinanga ‘Nandy’, Zuhura Othman ‘Zuchu’ na Paula Kajala, zawadi ya ubalozi wa taulo za wanawake Ora.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati alipotangazwa kuwa balozi wa taulo hizo, Priscilla alisema wasanii hao ndio anawapenda na wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki, hivyo aliona ni vyema kuwapa zawadi hiyo.

“Nashukuru Watanzania kwa kunipa ubalozi wa Ora. Naamini nitakuwa balozi mzuri na bidhaa hii itajulikana kimataifa. Wasanii niliowataja ni watu ambao nawapenda, na ndio maana nimewachagua kuwapa zawadi ya taulo za wanawake,” alisema Priscilla.

Kwa upande mwingine, Zamaradi Mketema, ambaye ni mshiriki kibiashara wa taulo za Ora, alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa kike kuhusu hedhi na umuhimu wa kutumia taulo za kike katika afya. SOMA: Jux asogeza mbele uzindua wa albamu

“Wanafunzi wa kike tutawapatia elimu kuhusu matumizi ya taulo, ili wajue kuwa kupata hedhi si jambo la aibu wala la kushangaza, bali ni jambo la kujivunia,” alisema Zamaradi.

Naye Mwakilishi wa Ora Comfort, Isaya, alisema kuwa wameleta bidhaa hii kwa Watanzania kwa kuwa ni nzuri na ina harufu nzuri, na inawafanya wanawake na mabinti kujiamini wanapokuwa wameivaa.

 

The post Mchumba wa Jux apewa ubalozi wa taulo za kike Ora appeared first on HabariLeo.