MIAKA 12 iliyopita, Titus Ngamau almaarufu Katitu, alikuwa afisa wa polisi aliyeogopwa sana.
Leo, Katitu hutegemea sana mapato kutoka kwa bendi yake ya Kithangaini Lipua Lipua akijaribu kujenga upya maisha yake baada ya kuachiliwa kutoka Gereza Kuu la Kamiti, ambako alifungwa kwa miaka sita.
Maisha yalibadilika mnamo 2013 baada ya kumpiga risasi Kenneth Kimani, ambaye afisa huyo wa polisi alidai alikuwa mshukiwa wa uhalifu huko Githurai, hatua ambayo ilimtumbukiza katika mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kufungwa kwake 2018 baada ya Jaji James Wakiaga kumpata na hatia ya kutumia vibaya silaha.
Baada ya kuachiliwa huru miezi miwili iliyopita, Katitu aligeukia muziki wa benga ili kujikimu kimaisha. Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 51, mtunzi wa nyimbo na mpiga gitaa anategemea bendi ya muziki ambayo wanachama wake wakuu ni watoto wake.
"|Ni mwanangu ambaye alinitambulisha kwa wateja wangu wengi wa sasa," aliambia Taifa Leo akimzungumzia mwanawe mkubwa Mwaniki ‘Kitolongwe’ Ngamau, 25, ambaye aliongoza bendi babake alipokuwa gerezani.
Elizabeth Mumbua, 23, ni mwimbaji na anapiga gitaa la rithimu huku Pius Kivuva, 21, akipiga gitaa la bezi na solo kando na kuwa mwimbaji. Michael Kasyoki, mzaliwa wa mwisho ambaye alisherehekea miaka 18 ya kuzaliwa Juni, anacheza gitaa la bezi.
"Muziki uko katika damu ya familia yetu,” Katitu anasema.Katitu anasema alirithi kipawa chake cha muziki kutoka kwa babake, Peter Musila, ambaye alikuwa mwanamuziki mashuhuri wa benga Ukambani akiongoza Bendi ya Kithangaini Brothers miaka ya 1970.
Afisa huyo wa polisi wa zamani anaweza kuwa na hamu ya kuimba wimbo mpya katika maisha yake, lakini kivuli cha maisha yake ya zamani linamwandama.
Miaka saba baada ya kuhukumiwa, Katitu amesalia kuwa kipenzi kwa baadhi ya watu kwa mbinu zake za kukabiliana na uhalifu huku wengine wakimchukulia kuwa mhalifu.
Hata hivyo, anasitasita kuzungumzia jambo hilo, akiahidi bila kufafanua kwamba atafunguka wakati ufaao.'Tusilizungumzie hilo sasa,' aliambia Taifa Leo alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwake, kushtakiwa na hatimaye kusukumwa jela.
IMETAFSIRIWA NA BENSON MATHEKA
Katitu, polisi aliyeogopwa sana ategemea muziki baada ya kutoka jela
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EntertainmentSherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo. Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria. Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria. Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa. Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao. Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe. Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja. Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja. Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja. Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza. Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.
EntertainmentVP agrees to become basketball patron, names Alikiba, Harmonize as influential figures
DAR ES SALAAM: VICE President Deogratius Ndejembi, has agreed to become the patron of basketball in the country, expressing his passion for the sport and his ambition to see it achieve popularity comparable to football. He urged artists and businesspeople to invest in basketball by owning teams, saying greater private investment would increase competition and…
EntertainmentTJ Vybez expands creative footprint with cinematic visual for ‘YAWA’
By Benjamin Njoku Rising Afrosounds star TJ Vybez is steadily carving out his own lane in Nigeria’s competitive music scene with a sound built on confidence, relatable storytelling and contemporary African rhythms. The singer, who has to his credit songs like ‘Illegal”, “Myself”, “Available” and ‘Baddie” from his EP “I Must Succeed” is expanding his […]
EntertainmentA saint has joined the angels – Tope Alabi mourns Toluwanisings
Nigerian gospel singer Tope Alabi has expressed sadness over the passing of gospel artiste Olayemi Bolaji, popularly known as Toluwanisings, who died at age 41.