TUNAPOTUNGA sentensi za Kiswahili, usahihi wa maneno ni muhimu sana.
Iwapo neno lililotumiwa katika sentensi litaandikwa visivyo, linaweza kusababisha sentensi kuwa na maana isiyokusudiwa na mwandishi.
Mojawapo wa makosa yaliyozoeleka katika uandishi wa maneno ni kudondosha baadhi ya konsonanti h na m katika maneno.
Aghalabu utapata sentensi kama vile:
*Tulimsaidia mama kuosha vyombo alafu tukaenda kucheza.
*Wanafunzi wote waliwasili shuleni asubui.
*Nilipofika nyubani nilimpata baba akifyeka nyasi.
*Mjoba aliuza buzi watano jana.
Mifano hii ya sentensi ina maneno *alafu, asubui, nyubani, mjoba, buzi ambayo si sahihi.
Konsonanti h imedondoshwa katika neno halafu na asubuhi.
Ili kusahihisha sentensi hizo tunafaa kuandika: Tulimsaidia mama kuosha vyombo halafu tukaenda kucheza. Wanafunzi wote waliwasili shuleni asubuhi.
Katika sentensi ya tatu na ya nne, maneno *nyubani, mjoba na buzi yamedondosha konsonanti m. Tunafaa kuandika: Nilipofika nyumbani nilimpata baba akifyeka nyasi. Mjomba alinunua mbuzi watano jana.
Udondoshaji wa herufi hizi aghalabu husababishwa na athari ya lugha ya kwanza hasa ikiwa konsonanti hiyo haipo katika lugha ambayo mwanafunzi alijifunza kwanza.
Mwanafunzi mwenye changamoto ya kudondosha baadhi ya konsonanti katika maneno anafaa kufanya mazoezi ya: kutambua konsonanti ambayo ana mazoea ya kuidondosha, kutamka maneno yenye konsonanti husika kwa sauti, kuandika sentensi mbalimbali akitumia maneno yenye konsonanti ambayo amezoea kudondosha katika maneno.
Tuendelee kujifunza Kiswahili ili kuimarisha mawasiliano.
Jinsi athari za lugha ya kwanza zinavyochangia makosa ya hijai

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
Jobs and CareerSanwo-Olu gives LASUED best graduate N5m, job
By Elizabeth Osayande Lagos State Governor, Babajide Sanwo-Olu, has rewarded the overall best graduating student of the Lagos State University of Education (LASUED), Blessed Mercy Olawunmi, with N5 million and automatic employment. The award was announced on Thursday, November 19, during the institution’s maiden convocation ceremony held at its Oto/Ijanikin campus. Olawunmi, of the Department […]
Joburg tightens water restrictions as consumers face higher tariffs
Johannesburg residents face Level 2 water restrictions and higher tariffs starting in November and December as the city aims to reduce daily consumption by 200 million litres to ease pressure on the Rand Water supply.
Joburg Council could face interdict over Soweto revote
The People of Joburg party has approached the Gauteng High Court over an irregular recount in Soweto's Ward 31, threatening to interdict the city council's first sitting and stall coalition negotiations.
Jobs and CareerInternship drive faces execution reality check
The government is stepping up efforts to expand employment opportunities for young Tanzanians, with plans to provide 30,000 internship placements while addressing gaps in access to jobs, training and business opportunities.