Jay Melody kutoana jasho na Diamond, Alikiba TMA

Mtanzania
Published: Aug 29, 2024 12:13:27 EAT   |  Entertainment

Na Mwandishi Wetu Kamati ya Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) leo Agosti 29,2024 imetangaza wanaowania tuzo za muziki nchini, wakianza na vipengele vitatu ambavyo ni ni Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, wimbo bora wa taarabu wa mwaka na wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi. Katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa mwaka, […]

Na Mwandishi Wetu

Kamati ya Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) leo Agosti 29,2024 imetangaza wanaowania tuzo za muziki nchini, wakianza na vipengele vitatu ambavyo ni ni Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, wimbo bora wa taarabu wa mwaka na wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi.

Katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa mwaka, wanaowania ni Marioo kupitia wimbo ‘Shisha’, Diamond Platnumz ‘Shuu’, Harmonize ‘Single Again’, Alikiba ‘Sumu’ na Jay Melody wimbo wa ‘Nitasema’.

Diamond Platnum

Vipengele vingine vilivyotangazwa ni wimbo bora wa taarabu wa mwaka ambapo kuna wimbo wa ‘Watu na Viatu’ wa Malkia Layla Rashid, ‘Hatuachani’ ya Amina Kidevu, ‘Bila Yeye Sijiwezi’ ya Mwinyi ‘Mkuu, Sina Wema’ ya Mwasiti Mbwana na ‘DSM Sweetheart’ ya Salha.

Wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi kuna ‘People’ ya Libianca, ‘American Love’ ya Qing Madi, ‘Lonely at the Top’ ya Asake, ‘Unavailable’ ya Davido ft Musa Keys na ‘Mnike’ ya Tyler ICU.

Alikiba

Kamati ya Tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha wamesema vipengele vingine vitaendelea kutangazwa, huku mashabiki wakitakiwa kujindaa kuwapigia kura wasanii wao wanaowapenda kuanzia Septemba 3,2024.