DAR ES SALAAM; Watanzania wametakiwa kuweka utamaduni wa kujiwekea akiba ili ziweze kuwasaidua siku za usoni.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa na Biashara za Kiserikali wa Benki ya Azania, Samson Mahimbi wakati akizindua kampeni ya Piga Ndeefu yenye lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, yakitarajiwa kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika sekta za utalii, malazi, usafiri na huduma nyingine.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam, amesema kampeni hiyo inalenga kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuchochea shughuli za kiuchumi zitakazowanufaisha Watanzania wakati wa maandalizi na kipindi cha mashindano ya AFCON 2027.
Mahimbi amesema kupitia kampeni hiyo, wateja watapata fursa ya kuweka akiba huku wakinufaika na riba pamoja na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
Amesema wateja wanaweza kuanza kuweka akiba kwa kiasi cha shilingi 500,000 na kupata riba ya hadi asilimia 12 kwa mwaka, kwa mujibu wa masharti ya kampeni hiyo.
Aidha, zawadi zitakazotolewa kwa washindi ni pamoja na tiketi za kushuhudia mechi ya ufunguzi na fainali za AFCON 2027, simu janja, televisheni na fedha taslimu.
Kampeni ya Piga Ndeefu itaendelea hadi Julai 21, 2027, huku Benki ya Azania ikilenga kuwahamasisha Watanzania kutumia fursa hiyo kujiwekea akiba na kuimarisha uwezo wao wa kifedha.
Benki hiyo pia inalenga kupitia kampeni hiyo kuongeza fursa za upatikanaji wa mitaji kwa biashara katika sekta mbalimbali zitakazochangia shughuli za kiuchumi zinazohusiana na maandalizi na uendeshaji wa mashindano ya AFCON 2027.
Benki ya Azania yajiweka mguu sawa AFCON 2027
DAR ES SALAAM; Watanzania wametakiwa kuweka utamaduni wa kujiwekea akiba ili ziweze kuwasaidua siku za usoni. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa na Biashara za Kiserikali wa Benki ya Azania, Samson Mahimbi wakati akizindua kampeni ya Piga Ndeefu yenye lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa…

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
SportsTPA yabeba medali tisa riadha Moro
MOROGORO: TIMU ya riadha ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imehitimisha kwa mafanikio katika mchezo wa riadha kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) 2026, yanayoendelea mkoani Morogoro kwa kutwaa jumla ya medali tisa. Katika mashindano hayo, TPA imefanikiwa kujinyakulia medali tatu za dhahabu,…
SportsEquity Group CEO on dividends, growth amid cyber threats and rising profits
'We have shown our ability to replicate returns made in Kenya in new markets in a shortened time.'
SportsSimba Corp eyes up to 20pc cut in MG car prices in local assembly
Simba Corp is MG’s exclusive distributor in Kenya and has until now been importing its internal combustion engine (ICE) and electric cars fully built.
SportsPolisi,Yanga kesho ni vita ya pointi tatu Ushirika
VITA ya pointi tatu inatarajiwa kupamba moto kesho Ijumaa, Novemba 20, wakati Polisi Tanzania itakapoikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, huku kila timu ikiwa na kiu ya kuhitaji ushindi.