WAKAZI wa mji wa Bomet wanakabiliwa na tatizo kubwa baada ya kaunti hiyo kukosa jaa rasmi la kutupa taka. Hali hiyo imesababisha mapipa ya taka katika sehemu mbalimbali za mji kurundika uchafu huku harufu mbaya ikisumbua wakazi na wafanyabiashara.
Tatizo hilo lilizuka baada ya jaa la muda lililokuwa likitumika kwa miaka 12 karibu na nyumba 220 za bei nafuu kufungwa kabla ya ziara ya Rais William Ruto mnamo Septemba 4. Inadaiwa kuwa eneo hilo lilifungwa kwa idhini ya Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (Nema).
Mkurugenzi wa Nema katika Kaunti ya Bomet, Richard Kering, alikiri kuwa mji huo hauna jaa lililoidhinishwa rasmi. Alisema serikali ya kaunti imekuwa ikichelewesha kutenga eneo linalokidhi masharti ya mazingira.
Kutokana na ukosefu wa jaa, wafanyakazi wa kaunti wamekuwa wakichoma taka usiku ili kupunguza mrundikano wa taka katika mapipa ya mji.
Mwenyekiti wa tawi la Bomet la Chama cha Wafanyabiashara nchini Kenya, Leonard Langat, alionya kuwa hali hiyo ni janga linalosubiri kulipuka, hasa wakati huu ambapo mvua ya El Niño inatarajiwa kuanza mwezi ujao.
Wanafunzi wa Bomet University pia wamepinga mpango wa kuanzisha jaa jipya karibu na chuo hicho na Mto Nyangores, ambao ni chanzo muhimu cha maji kwa wakazi na wanafunzi.
Gavana Hillary Barchok amekiri kuwa kaunti hiyo inakabiliwa na tatizo la afya ya umma na kusema juhudi zinaendelea kutafuta suluhisho la kudumu.
Balaa kaunti ikikosa jaa la taka

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessWafanyabiashara Moro wahamasishwa malipo kidigitali
MOROGORO:BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewahimiza wafanyabiashara nchini kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali katika manunuzi na mauzo ya bidhaa zao, ikieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya mzunguko wa fedha katika uchumi na kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na kubeba fedha taslimu. Rai hiyo imetolewa na Ofisa wa BOT kutoka Kurugenzi ya Mifumo…
BusinessWhy Ajaokuta remains moribund after 40 years — NES president
By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The President of the Nigerian Economic Society (NES), Dr. Baba Musa, has attributed the continued failure of the multi-billion-dollar Ajaokuta Steel Company to the absence of sustained long-term development plans. Musa said this at the 2026 National Growth and Development Forum (NGDF), with the theme, “The Nigeria We Want: […]
BusinessBoT yaimarisha ujumuishi wa kifedha kwa walemavu
IRINGA: Walemavu mkoani Iringa wameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa elimu ya fedha inayowasaidia kuelewa utunzaji sahihi wa fedha, matumizi ya mikopo na namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti, huku wakiiomba benki hiyo kupanua wigo wa mafunzo hayo ili yawafikie walemavu wengi zaidi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini. Pongezi hizo…
BusinessMuseveni, Samia push railway link to DRC
This could reshape trade routes into the Great Lakes region.