KATIBU Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Kutetea Masilahi ya Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli amelalamika kuwa licha ya uchumi wa Kenya kukua, mamilioni ya watu bado hawana ajira na maelfu ya wengine wamekimbilia sekta ya jua kali kujikimu kimaisha.
Akihutubia kikao cha 113 cha Kongamano la Shirika la Kimataifa la Leba jijini Geneva, Uswizi Jumatano, Bw Atwoli alisema idadi kubwa ya vijana wasio na ajira Kenya ni tishio kwa taasisi za utawala zinazolaumiwa kwa kufeli kutoa nafasi bora za ajira na njia nyinginezo za kuwawezesha kuchuma mapato.
“Nchini Kenya, sawa na katika nchi zingine zinazoendelea katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara, ukuaji wa kiuchumi haujazalisha nafasi za ajira. Zaidi ya watu milioni 5 hawana ajira na maelfu ya wengine wako katika sekta ya juakali. Asilimia 80 ya wasio na ajira wamekimbilia katika sekta hii,” Bw Atwoli akasema.
Katibu huyo mkuu alisema ongezeko la idadi ya watu wasio na ajira limechochea idadi kubwa ya Wakenya kuelekea mataifa ya ng’ambo kusaka ajira. Idadi kubwa huelekea katika mataifa ya Ghuba, Uropa na Amerika Kaskazini, ambako alisema mazingira mabaya ya kufanyia kazi.
“Malalamishi kuhusu ukiukaji wa haki za wafanyakazi yanaendelea kuripotiwa katika mataifa ya ng’ambo ambako Wakenya wanafanyakazi; haswa Uarabuni. Haya na mengine ndio shida ambazo Wakenya hupitia,” Bw Atwoli akaeleza.
Kulingana na kiongozi huyo wa COTU, misukosuko ya kisiasa katika baadhi ya mataifa ya Kiarabu na vita ni changamoto zingine zinazowakumba Wakenya wanaofanya kazi ughaibuni.
“Tangu Shirika la Kimataifa la Leba lilipobuniwa mnamo 1919, tumekuwa tukielekeza juhudi nyingi katika kuhakikisha kuwa ukuaji wa kiuchumi unazalisha nafasi za ajira zenye hadhi ambako haki za wafanyakazi zinalindwa,” Bw Atwoli akaeleza.
Atwoli alalama kuwa ukuaji wa uchumi wa Kenya hauzalishi ajira
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
Jobs and CareerSanwo-Olu gives LASUED best graduate N5m, job
By Elizabeth Osayande Lagos State Governor, Babajide Sanwo-Olu, has rewarded the overall best graduating student of the Lagos State University of Education (LASUED), Blessed Mercy Olawunmi, with N5 million and automatic employment. The award was announced on Thursday, November 19, during the institution’s maiden convocation ceremony held at its Oto/Ijanikin campus. Olawunmi, of the Department […]
Joburg tightens water restrictions as consumers face higher tariffs
Johannesburg residents face Level 2 water restrictions and higher tariffs starting in November and December as the city aims to reduce daily consumption by 200 million litres to ease pressure on the Rand Water supply.
Joburg Council could face interdict over Soweto revote
The People of Joburg party has approached the Gauteng High Court over an irregular recount in Soweto's Ward 31, threatening to interdict the city council's first sitting and stall coalition negotiations.
Jobs and CareerInternship drive faces execution reality check
The government is stepping up efforts to expand employment opportunities for young Tanzanians, with plans to provide 30,000 internship placements while addressing gaps in access to jobs, training and business opportunities.