Video
ASITISHIWA SAFARI BAADA YA KUENDESHA KWA ZAIDI YA SAA 15 BILA KUPUMZIKA
Channel: ITV Tanzania Watch on YouTube
About this video
Wakati sikukuu za mwisho wa mwaka zikikaribia, makamanda wa vikosi vya usalama barabarani kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa wameungana kufanya operesheni ya pamoja ya kukagua vyombo vya moto usiku na mchana, ikiwemo kuwapima madereva kubaini matumizi ya vilevi, kwa lengo la kuimarisha usalama wa watumiaji wa barabara na kuhakikisha wananchi wanasafiri salama kuelekea mwaka 2026. Operesheni hiyo inafanyika katika barabara ya Singida–Mwanza, eneo la Nala jijini Dodoma, ikihusisha ukaguzi wa mabasi ya abiria, magari madogo, magari makubwa na malori, sambamba na utoaji wa elimu ya usalama barabarani. Katika ukaguzi huo, baadhi ya mabasi yamebainika kutokuwa na mikanda ya usalama na kuchukuliwa hatua kwa kutozwa faini. Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, kiongozi wa operesheni hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Yussuph Kamotta, ameeleza kuwa ukaguzi huo ni sehemu ya mikakati ya kudhibiti makosa yanayoweza kusababisha ajali na kuhatarisha maisha ya wasafiri. Katika hatua nyingine, dereva Job Mbawala amezuiwa kuendelea na safari baada ya kubainika kuwa alikuwa akiendesha gari kwa zaidi ya saa 15 bila kupumzika, akitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama. Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na hatari inayoweza kusababishwa na uchovu wa dereva kwa maisha yake pamoja na watumiaji wengine wa barabara. Operesheni hiyo inalenga kuhakikisha madereva wanazingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, hasa katika kipindi hiki ambacho idadi ya wasafiri huongezeka kutokana na maandalizi ya sikukuu za mwisho wa mwaka.
Related stories
Travel
TravelTANAPA , YALENGA KUINUA UTALII WA NDANI
TravelIndia prepares to launch new low-cost airline in May 2027
Founded by entrepreneur Srinivas Chilukuri, the Andhra Pradesh-based venture is backed by a proposed investment of approximately ₹390 crore and aims to improve air connectivity between Tier-2 and Tier-3 cities.
TravelHow safe are National Parks in East Africa? In case one gets lost in there for days
Helicopters and drones have been dispatched to search for a missing person in the Aberdare National Park of Kenya