SAFARI ya mbali huanza kwa hatua moja, ni kauli anayoienzi Francis Thoya ambaye hutengeneza vitafunwa kwa kutumia bidhaa za kula ambazo huishia kutupwa kwa wasioona thamani yazo.
Kilichoanza kwa kuchakata kilo moja ya vitafunwa vya samaki kwa jiko dogo kimestawi na kuwa biashara inayounganisha wakulima kupitia uongezaji thamani, huku ikilenga kukabiliana na changamoto za lishe eneo la Pwani.
Kupitia EcoAfia Initiative, Thoya anasindika samaki, mihogo, moringa, njugu, korosho, nazi na mabuyu, akiunda bidhaa za kula zilivyosheheni virutubisho. Biashara iko Kilifi, ambapo inashirikiana na karibu wakulima 500 walio kwenye makundi 10, wengi wao wakiwa wanawake.
“Ni biashara changa na huzalisha kati ya kilo mbili hadi tano za vitafunwa kwa siku na hadi kilo 10 za bidhaa zilizoongezwa virutubisho,” Thoya anaiambia ‘Akilimali’. Licha ya mafanikio hayo, anasema mahitaji ya soko ni makubwa kuliko uwezo wake wa sasa wa uzalishaji.
Bidhaa za samaki
Aidha, hutengeneza aina tatu ya bidhaa—Samaki Cookie Magic Snack, Samaki Cookie Cycle Care inayolenga lishe ya wanawake, na Samaki Cookie Baby Nutrient, bidhaa iliyoongezwa virutubisho kwa minajili ya watoto. Samaki Cookie Baby Nutrient, ni unga unaotumika kuandaa uji. Kipakio cha gramu 250 ya Samaki Cookie huuza Sh50, huku Samaki Cookie Cycle Care moja ni Sh5.
[caption id="attachment_193137" align="aligncenter" width="300"] Francis Thoya, mwanzilishi wa EcoAfia Initiative katika Kaunti ya Kilifi, wakati wa Mkutano wa Vijana wa Kenya kuhusu Mifumo ya Kilimo na Chakula (KYASS) 2026, uliofanyika Kenya School of Government, Kabete, Nairobi, mnamo Septemba 2, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption]
EcoAfia Initiative ilianzishwa mwaka 2020 baada ya Kenya kukumbwa na janga la Covid-19. Thoya anasema “Nilinuwia kutumia raslimali za kilimo na baharini zinazopatikana Pwani kutengeneza bidhaa zenye thamani badala ya wakulima na wavuvi kuuza mazao na bidhaa zao kwa bei duni,” Thoya anaelezea.
Samaki Cookie, anadokeza kwamba ni kitafunwa kinachotengenezwa kwa mchanganyiko wa unga wa muhogo, unga wa samaki, moringa, njugu, korosho, nazi na mbegu za mabuyu.
“Wakulima wengi Kilifi wanajishughulisha na kilimo cha kujikimu mahitaji muhimu ya kimsingi, huku eneo hilo pia likikabiliwa na changamoto za chakula na lishe,” anasema.
Katika uchakataji wa samaki, anatumia sehemu ambazo kwa kawaida hutupwa, zikiwemo kichwa, magamba, matumbo na mifupa, ambazo hukaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga huo huchanganywa na viungio vingine kutengeneza vitafunwa na bidhaa zilizoongezwa virutubisho, huku zikisheheni virutubisho kama vile omega-3.
[caption id="attachment_193138" align="aligncenter" width="184"] Francis Thoya, mwanzilishi wa EcoAfia Initiative katika Kaunti ya Kilifi, akionyesha baadhi ya bidhaa zilizoongezwa thamani kwa kutumia samaki na mazao yanayostahimili mabadiliko ya tabianchi. Picha|Sammy Waweru[/caption]
Alvyoanza usindikaji
Thoya alianza biashara anayofanya kwa majaribio nyumbani kwa kutumia sufuria ndogo na hakuwa na mafunzo rasmi ya kuoka. Anasema alibadilisha mchanganyiko mara kadhaa baada ya jaribio la kwanza kuwa na harufu isiyopendeza. Baada ya miaka kadhaa ya majaribio na kupokea maoni kutoka kwa wateja, anasema alipata fomula maalum mwaka 2024.
Wahisani wamekuwa nguzo muhimu kufanikisha azma yake. “Nimepata usaidizi kutoka kwa baadhi ya wahisani na mashirika,” akasema wakati wa mahojiano.
Planet Ash ilimsaidia kupata jiko la kuoka, huku Farm Africa ikimnoa makali katika usindikaji wa samaki na uthibitishaji wa bidhaa.
Kwa sasa, changamoto kuu ni kupata vifaa vya kisasa kuongeza uzalishaji. Kifaa anachotumia, ndicho cha kukaushia samaki na kuoka vitafunwa, hivyo kupunguza kiwango cha uzalishaji. “Nikipata mashine na mitambo ya kisasa, itakuwa rahisi kuanzisha kiwanda cha uchakataji,” anaamini.
Changamoto nyingine ni athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo yanatishia wakulima na upatikanaji wa malighafi ya kutosha. Anahimiza wakulima kukuza mazao anayohimili mikumbo ya tabianchi. Hata ingawa soko lake kuu ni Kilifi, hupata oda kutoka Nairobi, Kisumu na Nanyuki.
Anatumia malighafi ya samaki kuunda vitafunwa

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
BusinessWafanyabiashara Moro wahamasishwa malipo kidigitali
MOROGORO:BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewahimiza wafanyabiashara nchini kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali katika manunuzi na mauzo ya bidhaa zao, ikieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya mzunguko wa fedha katika uchumi na kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na kubeba fedha taslimu. Rai hiyo imetolewa na Ofisa wa BOT kutoka Kurugenzi ya Mifumo…
BusinessWhy Ajaokuta remains moribund after 40 years — NES president
By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief The President of the Nigerian Economic Society (NES), Dr. Baba Musa, has attributed the continued failure of the multi-billion-dollar Ajaokuta Steel Company to the absence of sustained long-term development plans. Musa said this at the 2026 National Growth and Development Forum (NGDF), with the theme, “The Nigeria We Want: […]
BusinessBoT yaimarisha ujumuishi wa kifedha kwa walemavu
IRINGA: Walemavu mkoani Iringa wameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa elimu ya fedha inayowasaidia kuelewa utunzaji sahihi wa fedha, matumizi ya mikopo na namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti, huku wakiiomba benki hiyo kupanua wigo wa mafunzo hayo ili yawafikie walemavu wengi zaidi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini. Pongezi hizo…
BusinessMuseveni, Samia push railway link to DRC
This could reshape trade routes into the Great Lakes region.