SERIKALI imetenga ajira mpya 1,000 kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambazo zitatolewa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi alisema hayo mjini Morogoro jana akifungua kikao cha baraza dogo la wafanyakazi wa jeshi hilo.
Mkomi alisema ofisi hiyo inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha uboreshaji unafanyika kiutendaji hususani katika upatikanaji wa askari wapya.
“Kama ambavyo imeelezwa, tumetoa kibali cha watumishi wapya 425 na pia kwenye bajeti inayokuja (2025/2026), tumetenga watumishi wapya 1,000 na tunaangalia ukubwa wa majukumu tuliyokuwa na changamoto zilizoelezwa, nahisi hata hawa 1,000 hawatatosha,” alisema.
Mkomi alisema kuna ujenzi wa vituo vipya saba vya Zimamoto na Ukoaji na miradi ya kimkakati ambayo ni Kiwanja cha Ndege Msalato ambacho kinahitaji watumishi 164 wa jeshi hilo.
Alitaja mradi mwingine ni ujenzi wa kiwanja cha ndege mkoani Shinyanga ambacho kinahitaji watumishi 78 wa jeshi hilo. Vilevile kiwanja cha ndege Mtwara ambacho kimekamilika na kina watumishi wachache wa jeshi hilo.
Uongozi wa jeshi hilo ulisema kwa sasa wanahitajika watumishi 7,552.
“Maana yake, bado mahitaji ya watumishi ni kubwa zaidi na kila tunavyosonga mbele, mahitaji yanaongezeka,” alisema Mkomi.
Aliongeza: “Nimeambiwa kwenye SGR ambapo tumeanzia Dar es Salaam- Morogoro hadi Doodma , tunahitaji watumishi lakini mradi huo unaenda mbele zaidi na tutahitaji watumishi wengi zaidi.”
Alisema serikali kwa mwaka huu wa fedha imetenga watumishi wapya 425 na kibali lilichatolewa na jeshi hilo, kipo kwenye hatua za mchakato wa kuwapata na kwa mwaka ujao wa fedha 2025/2026 imetenga watumishi wapya 1,000.
Katibu mkuu pia alilitaka jeshi hilo wakati wa kufanya usaili wa kupata askari wapya, lifuate sheria, kanuni na utaratibu pasipokuweka upendeleo ili kuwapata askari wenye uwezo ndani ya jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Masunga alisema jeshi hilo linaendelea kuomba vibali vya ajira kila mwaka kutoka katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukabili upungufu wa rasilimaliwatu.
“Kwa mwaka 2024/2025, jeshi limepata kibali cha ajira kwa askari wapya 425 na taratibu za kuajiri askari hao zinaendelea,” alisema Masunga.
Alisema jeshi hilo limepokea Sh bilioni 2.6 kwa ajili ya kumalizia vituo saba vya zimamoto na uokoaji katika mikoa ya Simiyu, Kagera, Geita, Songwe, Katavi, Njombe na Manyara.
Pia, alisema Jeshi hilo limepokea Sh milioni 200 kwa ajili ya ukarabati wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Mkoa wa Morogoro.
The post Ajira 1,000 zaja Zimamoto na Uokoaji appeared first on HabariLeo.
Ajira 1,000 zaja Zimamoto na Uokoaji
This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
Jobs and CareerSanwo-Olu gives LASUED best graduate N5m, job
By Elizabeth Osayande Lagos State Governor, Babajide Sanwo-Olu, has rewarded the overall best graduating student of the Lagos State University of Education (LASUED), Blessed Mercy Olawunmi, with N5 million and automatic employment. The award was announced on Thursday, November 19, during the institution’s maiden convocation ceremony held at its Oto/Ijanikin campus. Olawunmi, of the Department […]
Joburg tightens water restrictions as consumers face higher tariffs
Johannesburg residents face Level 2 water restrictions and higher tariffs starting in November and December as the city aims to reduce daily consumption by 200 million litres to ease pressure on the Rand Water supply.
Joburg Council could face interdict over Soweto revote
The People of Joburg party has approached the Gauteng High Court over an irregular recount in Soweto's Ward 31, threatening to interdict the city council's first sitting and stall coalition negotiations.
Jobs and CareerInternship drive faces execution reality check
The government is stepping up efforts to expand employment opportunities for young Tanzanians, with plans to provide 30,000 internship placements while addressing gaps in access to jobs, training and business opportunities.