NA FRIDAH OKACHI MWANAMUZIKI wa mtindo wa Africapopster Nadia Mukami amejitokeza kulaumu Chama cha Hakimiliki za Muziki Nchini (MCSK) kwa kukosa kumpa pesa zake tangu mwaka 2017. Kwenye mahojiano na Taifa Leo, mwanamuziki huyo amelaumu uongozi wa Dkt Ezekiel Mutua katika MCSK akidai wanabagua wanamuziki nchini. Aidha alidai kwamba maafisa wa MCSK wameshindwa kueleza jinsi walivyotumia Sh56 milioni zilizokusanywa kutokana na […]