MSANII wa zamani wa injili na mshindi wa tuzo za Groove, Kevin Kioko almaarufu Bahati (Mtoto wa mama) amefunguka kuhusu kudidimia kwa muziki wa injili nchini katika miaka ya hivi karibuni.
Msanii huyo anasema Kenya itasalia kuwa ngome kuu ya wasanii wa injili japo kutakuwepo na changamoto ya kupata wasanii wakubwa kama ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.
Kwenye mahojiano na Taifa Dijitali, Bahati anaeleza kuwa kibali hicho kinang’aa nchini Nigeria na Rwanda. Alitaja wasanii wa injili waliopewa kibali hicho walianza majivuno, chuki miongoni mwao na kusababisha kusambaratika.
“Kenya ilikuwa na itazidi kuwa ngome ya injili lakini sio kama miaka 10 iliyopita. Kwa sababu Mungu amehamisha kibali hicho…” Alisema Bahati.
Baba huyo alisema kuwa wingi wa vipaji vilivyokuwa vimekuzwa kanisani vimegeuzwa na kuwa na chuki.
“Si kwamba Kenya hatujui kuimba vizuri, au hatuna nyimbo nzuri za injili, hapana. Ukweli ni kwamba vipaji vimebadilishwa,” aliongeza Bahati.
Msanii huyo alisisitiza kwamba idadi kubwa ya vibaraka wamo kanisani ikilinganishwa na wale wapo kwenye muziki wa kidunia.
“Wakati mtu unafanikiwa, watu wanajumuika pamoja kwa haraka ili kukuangusha katika sekta ya injili kuliko sekta ya Gengetone,” alieleza.
“Sipendi kuzungumzia sana kuhusu masuala ya kanisa. Najua wanajijua watasema natafuta kiki lakini ukweli ni kwamba mimi huogopa sana kusongea sekta ya injili kwa kuwa najua jinsi wanachukiana,” alisema.
Hata hivyo mtoto wa mama alikiri kuwa yeye si mwokovu sana kuliko walio mtandaoni, akihimiza kila mmoja kuomba msamaha na kunyenyekea kwa Mungu.
“Kitu najua tunahitaji kuomba msamaha na kuacha kuwa vibaraka ili Mungu atupeleke katika kiwango kingine. Bila hivyo, mimi naomba Mungu aendelee kuinua Arbantone kwa kujifanya manaibu wa Yesu,” alikamilisha.
Bahati alianza kuvuma mwaka wa 2010 akiwa sekta ya injili, mwaka 2015 akaanza kufanya kolabo na wasanii wa sekula. Hadi ilipofikia mwaka 2023 na kujitokeza na kuweka wazi kuwa si msanii wa injili.
Muziki wa injili utazidi kudidimia Kenya sababu vibaraka wamejaa, Bahati adai
This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
EntertainmentSherehe, muziki, ghadhabu Eldoret Sikukuu ya Mashujaa
MAELFU ya Wakenya walifurika katika Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret kusherehekea Sikukuu ya Mashujaa, huku muziki, gwaride la kijeshi, nyimbo za kizalendo na mavazi ya rangi za bendera ya taifa yakitawala hafla hiyo. Sherehe hizo za kitaifa pia ziligubikwa na hasira baada ya uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 kujaa kabla ya alfajiri, na kuwaacha maelfu ya wananchi nje licha ya kusafiri usiku kucha kuhudhuria. Kufikia saa tisa usiku, viti vilikuwa vimejaa, huku milango ikifungwa saa kumi na moja alfajiri. Waliokosa nafasi walilalamika kuwa walikuwa wamevumilia baridi kwa saa nyingi wakitarajia kushiriki hafla hiyo ya kihistoria. Ndani ya uwanja, burudani iliwafurahisha waliofanikiwa kuingia. Kundi la Maroon Commandos, kwaya za kitaifa na wasanii wa eneo hilo walitumbuiza, huku gwaride la kijeshi na maafisa wa vitengo mbalimbali vya usalama likivutia watazamaji. Watoto wa shule na watu wazima walishiriki kuimba nyimbo za kizalendo, huku bendera za Kenya zikipepea. Baadhi ya wananchi walijipamba kwa rangi nyeusi, nyekundu, kijani na nyeupe, huku wengine wakijifunika bendera za taifa. Lakini nje ya uwanja, hali ilikuwa tofauti kwa sababu polisi walikabiliana na umati uliotaka kuingia, huku baadhi ya wananchi wakilalamikia matumizi ya nguvu na kutengwa katika sherehe zilizokuwa zikifanyika katika eneo lao. Badala ya kukata tamaa, David Mutua, mkazi wa Kipkaren, aligeuza barabara kuwa ukumbi wa burudani kwa kutumia redio yake kubadilisha hali ya huzuni kuwa shangwe. Alipocheza nyimbo za kizalendo kama Tushangilie Kenya Taifa Letu Tukufu, Kenya ni Mama Yangu na Naipenda Nchi Yangu, wananchi walianza kuimba, kupiga makofi na kucheza pamoja. Bw Mutua alisema ingawa hawakuweza kuingia uwanjani, mapenzi yake kwa nchi hayangezuiliwa na kuta za uwanja. Sherehe hizo pia zilikuwa jukwaa la kuonyesha utamaduni wa jamii za Kalenjin huku wananchi kutoka Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet wakijitokeza kwa mavazi ya kitamaduni, nyimbo na ujumbe wa umoja. Hafla hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa kuwa kaunti hizo tatu zilikuwa zikishirikiana kuandaa sherehe za kitaifa kwa mara ya kwanza. Msongamano wa watu ulisababisha foleni barabarani, huku wafanyabiashara wakitumia fursa hiyo kuuza vyakula na bidhaa kwa wageni.
EntertainmentVP agrees to become basketball patron, names Alikiba, Harmonize as influential figures
DAR ES SALAAM: VICE President Deogratius Ndejembi, has agreed to become the patron of basketball in the country, expressing his passion for the sport and his ambition to see it achieve popularity comparable to football. He urged artists and businesspeople to invest in basketball by owning teams, saying greater private investment would increase competition and…
EntertainmentTJ Vybez expands creative footprint with cinematic visual for ‘YAWA’
By Benjamin Njoku Rising Afrosounds star TJ Vybez is steadily carving out his own lane in Nigeria’s competitive music scene with a sound built on confidence, relatable storytelling and contemporary African rhythms. The singer, who has to his credit songs like ‘Illegal”, “Myself”, “Available” and ‘Baddie” from his EP “I Must Succeed” is expanding his […]
EntertainmentA saint has joined the angels – Tope Alabi mourns Toluwanisings
Nigerian gospel singer Tope Alabi has expressed sadness over the passing of gospel artiste Olayemi Bolaji, popularly known as Toluwanisings, who died at age 41.