NA FRIDAH OKACHI VITA vya usimamizi wa umiliki wa muziki nchini vinazidi kuongezeka. Hivi punde, msimamizi wa mikakati ya kidijitali katika Ikulu Dennis Itumbi na afisa mkuu mtendaji wa chama cha kusimamia muziki Kenya (MCSK) Daktari Ezekiel Mutua wamerushiana cheche za maneno kwenye mtandao wa X (almaarufu Twitter). Bw Itumbi amemlaumu Bw Mutua kwa matumizi mabaya ya hela za wanamuziki […]