NA FRIDAH OKACHI RAPA Stephen Otieno almaarufu Stivo Simple Boy, amesema kuondoka kwa meneja wake ndio sababu ya yeye kuanguka wakati wa kipindi cha burudani cha ‘10 Over 10’ kinachopeperushwa na runinga ya Citizen. Mwanamuziki huyo alianguka mnamo Ijumaa. Kwenye mahojiano na Taifa Leo mnamo Jumamosi, alisema meneja wake aliondoka majuzi, hali ambayo “huniletea mawazo mengi”. […]