DAR ES SALAAM: MSANII wa kundi la Zabron Singers maarufu Marco, Joseph amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 22 katika Taasisi ya Moyo wa Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Akizungumza na HabariLeo mwimbaji mwenzake Japhet Zabron ambaye amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo.
“Nikweli Marco Japhet amefariki ni gafla tu mshtuko wa moyo alianza jumapili iliyopita ukiachana na Jumapili hii na alikuwa asumbuliwi chochote kipindi cha nyuma hii imekuaa gafla “.
Ikumbukwe kwamba kuna baadhi ya nyimbo za dini alizowahi kutoa kipindi cha uhai wake iliyofanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na sehemu mbalimbali kipindi yupo kwenye kundi la Zabron Singers kama “Upo Single”.The post Marco wa Zabron Singers afariki dunia first appeared on HabariLeo.