Jitayarishe kwa kazi bora ya muziki! Mkali wa Bongo Flava kutoka Tanzania, Billnass, ameachia bomu baada ya wimbo wake mpya kabisa, “Number One,” akimshirikisha mkali Mbosso! “Number One” ni muunganiko bora zaidi wa 2024  na sauti za kuvutia  wimbo ambao unapanda chati ya ngoma kali kwa msimu na mwezi wa malavidavi.
ikumbukwe kuwa baraza la sanaa la taifa BASATA limewahikuwatoza  mbosso na Billnass faini ya milion tatu 3 kila mmoja na kuwafungia kutojishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia jana November 04, 2023 kutokana na  wimbo wa AMEYATIMBA ya WHOZU ambao maudui yake yalitajwa kukiuka kanuni na maadili hivyo sasa wamekuja kivingine.
 
Isikilize hapa…