Wasanii 300 kunyakua tuzo za Trace Awards
DAR-ES-SALAAM : TUZO za Muziki za Afrobeat Trace Awards zinazotarajiwa kufanyika Februari 26, 2025 mjini Zanzibar, zitawakutanisha wasanii…
The post Wasanii 300 kunyakua tuzo za Trace Awards appeared first on HabariLeo.
DAR-ES-SALAAM : TUZO za Muziki za Afrobeat Trace Awards zinazotarajiwa kufanyika Februari 26, 2025 mjini Zanzibar, zitawakutanisha wasanii zaidi ya 300 wa kimataifa.
Tuzo hizi zinalenga kusherehekea ubunifu, mitindo, ubora wa muziki, na utamaduni wa Kiafrika unaovuma duniani kote.
Valerie Alexie, Mkuu wa Mahudhui kutoka Trace, alibainisha kuwa tukio hilo ni jukwaa la kimataifa linalowaleta pamoja wanamuziki, wabunifu, wajasiriamali, na washawishi kutoka Afrika na diaspora.
Pia, alieleza kuwa sherehe hiyo itaonyesha umuhimu wa mchango wa Kiafrika katika tasnia ya muziki na sanaa duniani.SOMA : TANZANIA yazindua tuzo za comedy award
Kwa mujibu wa Seven Mosha, mwakilishi wa Trace Awards, tuzo hizi zitasaidia kuutangaza muziki wa Bongo Fleva duniani kupitia makala na mafunzo yatakayowawezesha wasanii kujifunza jinsi ya kuendesha biashara ya sanaa kwa mafanikio.
Kura za washindi wa vipengele 26 vya tuzo hizi zitafungwa Februari 15, 2025. Yahya Mohamed, Afisa Mkuu wa Mahudhui wa Azam Media, amesema ushirikiano huo utawezesha kurusha tukio hilo moja kwa moja na kuhakikisha ubora wa hali ya juu.
Tukio hili linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu kwa wasanii wa Kiafrika na kimataifa kuonyesha umahiri wao na kuchangia ukuaji wa muziki wa Kiafrika kwenye anga za kimataifa.
The post Wasanii 300 kunyakua tuzo za Trace Awards appeared first on HabariLeo.