Ramovic amchomoa Ikanga Speed
WAKATI mashabiki wa Yanga wakiwa na hamu kubwa ya kumuona nyota mpya wa kikosi hicho, Jonathan Ikangalombo 'Ikanga Speed' katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la (FA), dhidi ya Copco FC, mambo yamekuwa ni tofauti baada ya kukosekana baada ya kocha Sead Ramovic kumchomoa kikosini.