Mwinyi: Vyuo vikuu vijikite kwenye tafiti zenye tija kwa jamii

Habari Leo
Published: Jan 25, 2025 11:51:51 EAT   |  News

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amevikumbusha vyuo vikuu vilivyopo nchini…

The post Mwinyi: Vyuo vikuu vijikite kwenye tafiti zenye tija kwa jamii appeared first on HabariLeo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amevikumbusha vyuo vikuu vilivyopo nchini umuhimu wa kujikita katika kufanya tafiti ambazo zitatoa ufumbuzi wa changamoto za kijamii na kuzisambaza kwa watumiaji.
Rais Dk Mwinyi ameyasema hayo katika Mahafali ya 24 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait Chukwani Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Hussein Ali Mwinyi.
Ametoa wito kwa viongozi wa vyuo vikuu kuendelea kujenga uwezo wa kufanya tafiti kwa wafanyakazi kwa kutumia fursa ziliyopo pamoja na kushirikiana na vyuo vikuu vya vyengine vyenye wataalamu waliobobea katika tafiti kwa ajili ya kuwajengea uwezo wataalamu wazalendo.
SOMA: Rais Mwinyi atunukiwa Shahada ya Heshima Zanzibar
Dk Mwinyi ameeleza kuwa ni muhimu kwa Wizara na Idara za Serikali kushirikiana na vyuo vikuu kufanya tafiti na kutumia tafiti mbalimbali kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
Amesema Serikali inathamini juhudi za Chuo Kikuu cha Abdulrahnan Al Sumait katika utoaji wa elimu kwani kunachangia nguvu kazi na ongezeko la waatalamu wazalendo katika sekta mbalimbali za umma na kijamii.
Rais huyo wa Zanzibar ameahidi Serikali kuendelea kutoa ushirikiano wa kiwango cha juu ili chuo hicho kifikie malengo ya kuanzishwa kwake.
Wahitimu 304 katika fani mbalimbali mwaka wa masomo 2023-2024, wanawake wakiwa 203 na wanaume 101 na kufikisha wahitimu 4,993 kutoka chuo hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998.

The post Mwinyi: Vyuo vikuu vijikite kwenye tafiti zenye tija kwa jamii appeared first on HabariLeo.