Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Rwanda, Israel Mboni, atua Tanzania kwa huduma ya Uimbaji
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Rwanda, Israel Mboni, anayefahamika kwa wimbo wake maarufu Nina Siri, amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma katika matamasha ya uimbaji yanayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Novemba. Matamasha hayo yamepangwa kufanyika Novemba , 2024 katika Ukumbi wa Mlimani City na Novemba 3 katika Viwanja […]
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Rwanda, Israel Mboni, anayefahamika kwa wimbo wake maarufu Nina Siri, amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma katika matamasha ya uimbaji yanayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Novemba.
Matamasha hayo yamepangwa kufanyika Novemba , 2024 katika Ukumbi wa Mlimani City na Novemba 3 katika Viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari, Mboni alisema kuwa anafurahi kuja Tanzania na anawapenda sana Watanzania.
“Nimekuja kutoa huduma ya uimbaji. Tutaimba na kucheza pamoja, na naamini Watanzania watafurahia matendo makuu ya Mungu. Wote wajitokeze kwa wingi ili kubarikiwa na kazi ya Mungu nitakayofanya,” alisema Mboni kwa furaha.
Muandaaji wa ibada hiyo, Lilian Mkumbo, amewahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kushiriki na kufurahia ibada hiyo ya kipekee, huku akieleza kuwa mwitikio umekuwa mzuri na Watanzania wamepokea kwa shauku huduma hiyo.
Kwa upande wake, mwimbaji wa Injili kutoka Tanzania, Rehema Semfukwe, alieleza furaha yake kutokana na mapokezi aliyoyapata Mboni kwenye uwanja wa ndege na kuwataka Watanzania kutokosa ibada hiyo ya kipekee.
“Husipange kukosa baraka hizi kubwa katika ibada hii. Njooeni tuimbe, tucheze, na tumshukuru Mungu kwa pamoja. Wote mnakaribishwa,” alisema Semfukwe.
Israel Mboni atasindikizwa na wasanii maarufu wa Injili kutoka Tanzania, akiwemo Rehema Semfukwe, Paul Clement, Joel Lwaga, Boaz Danken, Upendo Nkone, Bella Kombo, na wengine wengi, ambao kwa pamoja wanatarajiwa kuleta msisimko na utukufu wa Mungu kwenye matamasha hayo.