Mora mwenyeji tuzo za trace Zanzibar

Habari Leo
Published: Oct 30, 2024 14:16:27 EAT   |  Entertainment

KAMPUNI kubwa ya muziki duniani na mpaishaji wa muziki wa Afrobeat, Trace, imetangaza kuwa itafanya toleo la 2025 nchini Zanzibar katika sherehe za tuzo za Trace zinazosherehekea ubunifu, mitindo na ubora wa muziki na utamaduni wa Kiafrika -unaosambaa duniani kote. Katika uzinduzi wa Tuzo za Trace uliofanyika asubuhi hii katika The Mora, Waziri wa Utalii …

The post Mora mwenyeji tuzo za trace Zanzibar first appeared on HabariLeo.

KAMPUNI kubwa ya muziki duniani na mpaishaji wa muziki wa Afrobeat, Trace, imetangaza kuwa itafanya toleo la 2025 nchini Zanzibar katika sherehe za tuzo za Trace zinazosherehekea ubunifu, mitindo na ubora wa muziki na utamaduni wa Kiafrika -unaosambaa duniani kote.

Katika uzinduzi wa Tuzo za Trace uliofanyika asubuhi hii katika The Mora, Waziri wa Utalii wa Zanzibar, Mudrik Soraga, alizungumzia thamani ambayo Zanzibar itapata kutokana na kuangaziwa kimataifa kwa wanamuziki, wabunifu, wajasiriamali na washawishi kutoka Afrika na diaspora ya Kiafrika.

“Tuzo hizi ni njia yetu ya kusherehekea athari za muziki na viongozi wengine katika mandhari ya utamaduni wa kisasa duniani, na sherehe hii ya kiwango cha juu itadhihirisha umuhimu wa tuzo zinazotolewa na umahiri wa wasanii wa Kiafrika katika tasnia ya muziki na sanaa duniani. Wamechagua mahala bora kabisa duniani kwa tuzo hizi,” aliongezea.

Tuzo za Trace zitafanyika Zanzibar kuanzia 24 hadi 25, 2025, kwa ushirikiano na Wizara ya Utalii ya Zanzibar na zitafanyika katika The Mora Resort shukrani kwa Meneja Masoko wa hoteli hiyo, Bi. Porche Dumagude. “Hakuna mahali bora zaidi pa kufanyika usiku wa tuzo kuliko The Mora,” aliongeza.

“Tukio hilo litajumuisha sherehe ya muziki ya mubashara inayotangazwa kwa saa tatu ambayo inahitaji maeneo na majukwaa ya kiwango cha juu yanayofaa tukio kama hili. Sisi Showtime tuko tayari kusaidia tukio hili kwa uwezo wetu kiufundi usio na kifani,” amesema Ibrahim Mitawi, mmiliki wa kampuni ya Matukio na Burudani, Showtime, kampuni inayoongoza ya usimamizi wa matukio ya kijamii Tanzania.

Kampuni ya Showtim ya Zanzibar, imekuwa ikisimamia matukio makubwa ya kimataifa na hili linakidhi uwezo wake kwani wana miliki vifaa bora vya kiufundi kwa muziki na maonyesho mubashara nchini.

Tukio hilo litajumuisha maonyesho kutoka kwa wasanii wakubwa wa Kiafrika na wa asili ya Afrika duniani, na litafanyika mbele ya mashabiki 7000 wa muziki, wanamuziki, washawishi, wabunifu wa mitindo na watunga sera kutoka Afrika na duniani kote. Tuzo hizi zitasimamia aina mbalimbali za muziki kutoka Afrobeat hadi Dancehall, Afro-pop, Mbalax, Amapiano, Zouk, Kizomba, Genge, Coupé Décalé, Bongo Flava, Soukous, Gospel, Rap, Kompa, R&B, na Rumba, na kuwatunuku wasanii wa sanaa mbalimbali za kitamaduni.

Akizungumza katika tukio hilo, Mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa Trace Olivier Laouchez amesema, “Tumafurahi sana kuweza kuandaa Tuzo za Muziki za Trace hapa Zanzibar kwani tunaona tuzo hizi ni kama sherehe ya kimataifa ya utamaduni wa Kiafrika katika nchi hii nzuri na bora zaidi, ikitangaza Zanzibar kama kivutio cha utalii wa kitamaduni, na kuandaa matukio ya kiwango cha juu. Zanzibar na Tanzania zitakuwa jukwaa kubwa kwa sekta ya utalii kuonyesha vivutio vyake mbalimbali ikiwa ni pamoja na urithi wetu wa kitamaduni pamoja na Mji Mkongwe, ambao ni Eneo la Urithi wa Dunia.”

“Tuzo za Trace zitaonyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya Trace katika nchi zaidi ya 180 duniani kote,” alithibitisha Bi. Valerie Gilles-Alexia, Mkuu wa Maudhui, Mawasiliano na Ofisi ya CSR ya Tuzo za Trace, akiongeza kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa sahihi kwa wapenda muziki duniani.

“Sisi wa Showtime tuko tayari kuitangaza Zanzibar ulimwenguni,” ameongeza Mitawi wa Showtime.

The post Mora mwenyeji tuzo za trace Zanzibar first appeared on HabariLeo.