Adele achukua mapumziko ya muda mrefu kutoka kwenye Muziki

Milard Ayo
Published: Sep 02, 2024 10:03:18 EAT   |  Entertainment

Adele alihitimisha maonesho yake huko Munich Jumamosi kwa onyesho la 10 katika jiji la Ujerumani, ambapo alisisitiza mpango wake wa kupumzika kwa muda mrefu kutoka kwenye muziki kufuatia kumalizika kwa maonyesho yake ya Weekends With Adele huko Las Vegas msimu huu. “Nahitaji kupumzika tu. Nimetumia miaka saba iliyopita kujijengea maisha mapya na ninataka kuyaishi sasa,” […]

The post Adele achukua mapumziko ya muda mrefu kutoka kwenye Muziki first appeared on Millard Ayo.

Adele alihitimisha maonesho yake huko Munich Jumamosi kwa onyesho la 10 katika jiji la Ujerumani, ambapo alisisitiza mpango wake wa kupumzika kwa muda mrefu kutoka kwenye muziki kufuatia kumalizika kwa maonyesho yake ya Weekends With Adele huko Las Vegas msimu huu.

“Nahitaji kupumzika tu. Nimetumia miaka saba iliyopita kujijengea maisha mapya na ninataka kuyaishi sasa,” Adele akiwa na hisia kali aliuambia umati. “Nataka kuishi maisha yangu ambayo nimekuwa nikijenga na nitakukosa sana.”

“Lakini baada ya hapo, sitawaona kwa muda mrefu sana,” Adele alisema. “Na nitawashika moyoni mwangu kwa muda wote huo wa mapumziko.”

Katika mahojiano ya redio mwezi Julai, Adele alifichua kwanza kwamba angeacha muziki ili kuzingatia familia na “mambo mengine ya ubunifu” baada ya maonesho yake kumalizika

“Sina mpango wowote wa kufanya muziki mpya, hata kidogo,” Adele alisema mwezi uliopita. “Nataka mapumziko makubwa baada ya hili na nadhani nataka kufanya vitu vingine vya ubunifu, kwa muda mfupi tu.”

The post Adele achukua mapumziko ya muda mrefu kutoka kwenye Muziki first appeared on Millard Ayo.