Ruto ajipatia njia kukwepa kosa la Uhuru

NA ONYANGO K’ONYANGO RAIS William Ruto ameamua kusimamia masuala ya muungano wa Kenya Kwanza (KKA) kutumia mbinu ya mashauriano hali ambayo imemfanya kupata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge. Tofauti na mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta, ambaye wabunge walilalama kuwa ilikuwa vigumu kwao kumfikia, Rais Ruto aliamua kufungua milango yake kwa viongozi wote katika muungano wa KKA. […]