Mwili wa mlinzi wapatikana ndani ya darasa

Taifa Leo
Published: Nov 20, 2022 16:33:28 EAT   |  Educational

NA GEORGE MUNENE MWILI wa mlinzi wa Shule ya Msingi ya Kanjuu, eneobunge la Gichugu, Kirinyaga, jana Jumamosi ulipatikana ndani ya darasa ambalo halitumiki kwa shughuli za masomo. Wanafunzi ambao walikuwa wakicheza karibu na darasa hilo waliona mwili wa mlinzi huyo Peter Chomba Ndumbi, 62.