
Mukumu: Machogu aahidi fidia ya Sh400,000 kwa kila familia iliyopoteza mtoto
Published: May 31, 2023 09:27:31 EAT | Educational
NA COLLINS OMULO WAZIRI wa Elimu Ezekiel Machogu amesema familia za wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Sacred Heart Mukumu walioaga dunia baada ya kula chakula kibovu na kunywa maji machafu zitapokea fidia ya Sh400,000 kwa kila mwanafunzi aliyeangamia. Bw Machogu ambaye anahojiwa na Seneti amesema mpango huo utafanikishwa na bima ya afya ya EduAfya. […]