Makatibu: Mahakama yatupilia mbali kesi za kupinga bunge kuwapiga msasa watu 51

Taifa Leo
Published: Nov 29, 2022 09:36:20 EAT   |  News

NA RICHARD MUNGUTI MAHAKAMA ya Kuanua Mizozo ya Wafanyakazi na Waajiri imetupilia mbali kesi za kupinga bunge kuwapiga msasa watu 51 waliopendekezwa na Rais William Ruto kuwa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali. Jaji Mathew Nduma Nderi amesema kesi hizo zingewasilishwa baada ya uteuzi kamili kutekelezwa.