Mavunde awashika mkono mama lishe Stendi Kuu Dodoma

Habari Leo
Published: Apr 02, 2024 15:10:05 EAT   |  News

DODOMA: Mbunge wa Dodoma Mjini Athony Mavunde ameahidi kuwaboreshea mazingira ya utoaji huduma mama lishe wa Stendi Kuu Dodoma kwa kuwapatia meza nadhifu na vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya chakula. Mavunde ameyasema hayo leo Aprili 2, 2024 wakati wa mkutano wa wafanyabiashara wadogo,Mama Lishe na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa …

The post Mavunde awashika mkono mama lishe Stendi Kuu Dodoma first appeared on HabariLeo.

DODOMA: Mbunge wa Dodoma Mjini Athony Mavunde ameahidi kuwaboreshea mazingira ya utoaji huduma mama lishe wa Stendi Kuu Dodoma kwa kuwapatia meza nadhifu na vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya chakula.

Mavunde ameyasema hayo leo Aprili 2, 2024 wakati wa mkutano wa wafanyabiashara wadogo,Mama Lishe na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kutatua changamoto ya uhamishwaji wa wafanyabiashara hao katika maeneo ya stendi kuu Jijini Dodoma.

Mavunde amesema dhumuni la ujenzi wa stendi hiyo ni kutoa huduma ya usafirishaji na pia kuchochea uchumi wa wananchi wa Dodoma kupitia biashara mbalimbali.

“Nishauri uongozi wa Jiji kuwapangia utaratibu mzuri wafanyabiashara hawa wafanye biashara hii kwa muda na baadaye watarejea katika maeneo rasmi baada ya mzunguko wa biashara kuimarika sokoni hapa,”amesema na kuongeza.

“Nitawasaidia Mama Lishe meza nadhifu na vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ili msichafue mazingira hapa na mtoe huduma kwa kuzingatia kanuni za Afya na usafi wa Mazingira,”amesema Mavunde

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma John Kayombo amesema Jiji limekubali ushauri wa mbunge kwa masharti ya wafanyabiashara hao kupangwa vizuri na kusimamia usafi wa mazingira yao.

The post Mavunde awashika mkono mama lishe Stendi Kuu Dodoma first appeared on HabariLeo.