Watanzania wang’ara Kili Marathon 2023

Mtanzania
Published: Feb 26, 2023 17:21:22 EAT   |  Educational

*Waibuka kidedea mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili International Half Marathon 2023 Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Wanariadha wa Tanzania wameng’ara kwa kuibuka na ushindi wa kishindo katika Mbio za Kimataifa za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon 2023 zilizofanyika Februari 26, 2023 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) […]

*Waibuka kidedea mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili International Half Marathon 2023

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wanariadha wa Tanzania wameng’ara kwa kuibuka na ushindi wa kishindo katika Mbio za Kimataifa za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon 2023 zilizofanyika Februari 26, 2023 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) mkoani Kilimanjaro.

Katika mbio hizo mshindi kwa upande wa wanaume Watanzania wakiongozwa na Emmanuel Giniki walishika nafasi nne za kwanza ambapo Giniki alitumia muda wa saa 1:00:36.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Josephat Gisemo aliyekimbia kwa muda wa 1:05:12 akifuatiwa kwa Karibu na Decta Teziforce aliyekimbia kwa muda wa saa 1:05:43 na kushika nafasi ya tatu.

Afisa Mkuu wa Fedha kutoka Tigo,CPA. Innocent Rwetabura akimkabidhi mfano wa hundi,mshindi wa kwanza Tigo Kili International Half marathon(km 21) upande wa wanaume, Emmanuel Giniki

Katika hotuba yake baada ya mashindano hayo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa aliwapongeza washindi wa mbio hizo akisema kuwa mafanikio yao yameakisi matayarisho mazuri waliyoyafanya kabla ya kushiriki wao.

“Ushindi wenu ni chachu kwa wengine kujiandaa vyema mwakani ili wafanye vizuri na kwenu itakuwa mnawapa moyo wa kujituma zaidi ili kulinda mafanikio mliyoapata”, alisema.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mary Masanja, Mchengerwa alisema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na waratibu na wadau wengine wa mbio hizo kutokana na umuhimu wake kwa Taifa.