Tanzania inaongoza kwa biashara ya vinywaji-Dyre

Mtanzania
Published: Nov 28, 2022 14:43:02 EAT   |  Business

*Kuzindua Grand Tripple Wood’s 12 Kesho Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital BALOZI wa Grants Duniani, Danny Dyer, ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika biashara ya vinywaji ndio sababu imepewa heshima ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika, kuzindua kinywaji cha Grand Tripple Wood’s 12. Grand Triple woods 12, ni kinywaji kipya ambacho kinatengenezwa na […]

*Kuzindua Grand Tripple Wood’s 12 Kesho

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

BALOZI wa Grants Duniani, Danny Dyer, ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika biashara ya vinywaji ndio sababu imepewa heshima ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika, kuzindua kinywaji cha Grand Tripple Wood’s 12.

Grand Triple woods 12, ni kinywaji kipya ambacho kinatengenezwa na watengenezaji wa Grands tofauti ikiwa ni ladha na ubora.

Akizungumza Dar es Salaam leo Novemba 28, 2022, Balozi wa Grants duniani Dyer, kutoka Uingereza, amesema tayari kinywaji hicho chenye mchanganyiko wa matunda na vitu vitamu mfano wa pipi kimefika nchini na kinatarajiwa kuzinduliwa kesho Novembar 29.

“Tanzania imepata bahati ya kuwa nchi ya kwanza Afrika kufikiwa na kinywaji cha Grands Tripple Wood’s, ambacho kina ubora wa hali ya juu na ladha nzuri tofauti na vinywaji vingine,” anasema Danny.

Ameongeza kuwa kinywaji hicho kina ladha ya Vanila, Matunda na Asali uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa Element Masaki na kuhudhuriwa na watu mashuhuri kutoka tasnia tofauti.