Sanches ajipeleka Arsenal

Mtanzania
Published: Dec 08, 2021 08:19:57 EAT   |  Sports

LILLE, Ufaransa WASHIKA Bunduki wa London washindwe wenyewe! Ni baada ya kiungo wa Lille, Renato Sanches, kusema yuko tayari kujiunga nao endapo taratibu zote zitafuatwa. Sanches, raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akifukuziwa na klabu kadhaa za Ulaya baada ya kiwango kizuri alichokionesha katika fainali za Euro 2020. Lakini sasa, licha ya […]

LILLE, Ufaransa

WASHIKA Bunduki wa London washindwe wenyewe! Ni baada ya kiungo wa Lille, Renato Sanches, kusema yuko tayari kujiunga nao endapo taratibu zote zitafuatwa.

Sanches, raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akifukuziwa na klabu kadhaa za Ulaya baada ya kiwango kizuri alichokionesha katika fainali za Euro 2020.

Lakini sasa, licha ya kuonesha kuutamani ‘uzi’ wa Arseanl, changamoto kubwa kwa klabu hiyo ni ushindani kutoka kwa AC Milan inayomtolea macho mchezaji huyo.

Katika hatua nyingine, ipo stori inayodai kuwa winga wa Arsenal raia wa Ivory Coast, Nicolas Pepe, anajiandaa kuondoka Emirates ifikapo Januari, mwaka huu.