Jonathan Budju mbioni kuachia kitu kipya

Mtanzania
Published: Apr 01, 2024 16:57:00 EAT   |  Entertainment

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Staa wa muziki wa Injili nchini Canada, Jonathan Budju, mwishoni mwa wiki hii anatarajia kufanya video kwaajili ya wimbo wake mpya utakaotoka hivi karibuni. Budju ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Canada kwa mtindo wake wa Model Gospel, ameweka wazi kuwa wimbo huo utatoka chini ya lebo yake […]

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Staa wa muziki wa Injili nchini Canada, Jonathan Budju, mwishoni mwa wiki hii anatarajia kufanya video kwaajili ya wimbo wake mpya utakaotoka hivi karibuni.

Budju ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Canada kwa mtindo wake wa Model Gospel, ameweka wazi kuwa wimbo huo utatoka chini ya lebo yake ya Mastola Music.

“Nipo kwenye maandalizi ya kutoa wimbo wangu mpya ambao utakuwa out mwezi mmoja na nusu kutoka sasa, mashabiki wamekuwa na kiu ya kupata muziki mzuri kutoka kwangu,” amesema Budju anayetamba na wimbo Utukufu.

Jonathan Budju a.k.a Son of God ameendelea kuikumbuka jamii ya waafrika wenye uhitaji Afrika Mashariki kupitia taasisi yake ya JB Foundation.